Sep 17, 2013

Sheikh Ponda Anyimwa Dhamana.

 

Mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa Morogoro imemnyima dhamana katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.

Kwa mujibu taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka Morogoro zinasema hakimu Kabate amefikia maamuzi hayo kwa madai ya kwamba ni kwa maslahi ya usalama wake (sheikh ponda na maslahi ya taifa kwa ujumla bila ya kufafanua.

Akiifahamisha munira blog sheikh Abeid Haruob ambaye alikuwepo mahakamini alisema awali mahakamani hapo mawakili wa mshitakiwa walipinga hati ya kuzuwia dhamana iliyotolewa na DPP kwa madai kwamba ilitotolewa kwa njia za panya,lakini lakini hakimu alisema"licha ya madai yenu hati hii ina muhuri halali wa mahakama nami kama hakimu sina shaka na hati hii."

Aidha mahakama hiyo imepanga tarehe 01/10/2013 kutoa hukumu ya kesi ndogo  kufuatia madai ya upande wa mshitakiwa kwamba kwa kuwa moja ya mashitaka ni kukiuka masharti ya kifungo cha nje hukumu ambayo ilitolewa na mahakama ya kisutu,hivyo basi wenye mamlaka ya kushitaki ni mahakama ya kisutu na si Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.

0 comments:

Post a Comment