Oct 6, 2013

ISOMENI SAIKOLOJIA YA WATOTO-WITO

MTAALAMU WA SIKOLOJIA USTAADH JAMAL MARINGO AKIWASILISHA MADA KWA WANA SEMINA,HIVI PUNDE

Waalimu wanao fundisha Lugha ya Kiarabu wametakiwa kujikita katika somo la Saikolojia ya Watoto ili kurahisiha Uelewa.

Wito huo umetolewa leo hii na mtaalamu wa Saikolojia Ustaadh Jamal Maringo alipokuwa anawasilisha mada ya Saikolojia ya Elimu kwa washiriki wa semina ya walimu wa Madrasa katika somo la Lugha ya Kiarabu.

Alisema tabia za viumbe akiwemo mwanaadamu zinabadilika mara kwa mara,hivyo ni muhimu kujuwa chanzo cha mabadiliko hayo.

"Kujuwa chanzo cha tatizo kwa mtoto unaye mfundisha na kupata ufumbuzi wa tatizo lake ni sehemu ya Saikolojia",alisema.

"Itashangaza sana kuona kwamba mwanafunzi anakaa miaka mingi pasipo kumaliza juzuu amma,hili ni tatizo la mwalimu kutokuwa na elimu ya saikolojia ya elimu,kwani ufumbuzi wa tatizo hilo lina tatulika kwa kuwa na elimu ya saikolojia ya elimu".

Amesma Saikolojia ni pana mno,lakini Saikolojia ya elimu huwa ina ambatana na mambo matatu.

Aliyataja mambo hayo kuwa saikolojia ya elimu inamuangalia mwanafunzi,vitendo vya mwalimu na mazingira ya kufundishia.

Wakati huo huo Ustaadh Jamal Maringo aliwataka waalimu kupunguza adhabu badala yake kutoa adhabu za kitaaluma.

"Siyo kila kosa umchape mtoto,bali inawezekana kabisa ukatoa adhabu za kitaaluma na zikawa na mafanikio makubwa".Alisema.

"kama mwanafunzi kafanya makosa,mpe kazi ya kukuandikia sentesi mia moja za kiarabu,hapo itakuwa umemuadhibu kwa kuudhibiti muda wake lakini pia umemuimarisha kielimu".mwisho wa kumnukuu

Semina hiyo ya siku tatu itakayo malizika kesho,imeandaliwa na World Islamic Call Society,ina fanyika katika ukumbi wa Jaafar Complex uliopo Upanga Jijini Dar es salam.
BAADHO YA WANA SEMINA WAKIMFUATILIA MTOA MADA USTAADH JAMAL

0 comments:

Post a Comment