MKUU wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, amepiga marufuku walimu wa
shule za msingi na sekondari wilayani hapa kuwachangisha wanafunzi
michango ambayo ni kinyume na utaratibu wa Wizara ya Elimu. Mkuu huyo wa
wilaya alisema, yeyote atakayepuuza agizo lake na kuendelea kufanya
hivyo, sheria itachukua mkondo wake.
Aliyasema hayo wakati akipokea msaada wa madawati 100 kwa shule nne za msingi pamoja na matanki mawili ya kuhifadhia maji na vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 14.
Dendego alisema michango hiyo imewafanya baadhi ya wanafunzi kukosa masomo darasani, kufuatia kushindwa kuwasilisha michango ambayo iko kinyume na utaratibu.
“Kuanzia leo (jana) natoa agizo kwa walimu wote wa shule za msingi na sekondari kuacha kuwachangisha wanafunzi michango ambayo haiko kisheria na mwalimu atakayekwenda kinyume na agizo hili ofisi itamchukulia hatua za kisheria.
“Vitendo hivi vimepelekea wanafunzi wengi kuwa na matokeo mabaya darasani baada ya baadhi ya walimu kuwafukuza na kuachangia matokeo mabaya katika mitihani ya mwisho wa mwaka na ya kitaifa,” alisema.
Aliwataka kuyatumia maeneo ya shule kwa kulima kilimo cha mbogamboga na mazao ambayo yatawawezesha kuuza na kupata pesa ambazo zitaweza kulipia malipo ya maji na umeme pamoja na pesa za mlinzi, badala ya kuwachangisha wanafunzi.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake, Kaimu Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi ya Pande, Bakari Sesige, aliishukuru Rotary Club kwa msaada huo na kusema madawati hayo watayatunza na kutumika kama ilivyokusudiwa.

0 comments:
Post a Comment