Aug 20, 2013

WAISLAMU JITENGENI NA WANAOKUDHULUMUNI-SHEIKH KONDO.



 
SHEIKH KONDO BUNGO AKIONGEA NA WAISLAMU JUZI KATIKA 
VIWANJA VYA MWEMBE YANGA.

  • AKUMBUSHIA KUKWAMA KWA MAHAKAMA YA KADHI NA OIC.
  • SISI TUNAPUUZWA MAASKOFU WANASIKILIZWA
  • MZIGO KUUBADILISHA BEGA SIO KUPUNGUZA UZITO BALI…..

Na mwandishi wa wetu wa munira.
Waislamu nchini wametakiwa kujitenga mbali na wale wote wanaowafanyia dhulma katika nchi hii.

Hayo yamesemwa juzi na Sheikh Kondo bungo alipokuwa anaongea na Waislamu katika viwanja vya Mwembe Yanga vilivyopo Tandika Jijini Dar es salaam.

Amesema hakuna sababu ya kuwakumbatia wale wanaotudhulumu haki zetu,wanaotupiga virungu na risasi na wanao tuuwa pasipo hatia,kwani ni dhahiri hawatupendi na hatuna thamani kwao.

“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi haina usikivu kwa Waislamu wa Tanzania ,imekuwa inatupuuza kila kukicha madai,yetu yote wanatupilia mbali,lakini Serikali hii hii imekuwa mbele kuwasikiliza Maaskofu na Mapadri hadi kufikia kufanya nao makubaliano ya kuyapatia ruzuku Makanisa yote nchini Tanzania kila mwaka hali ya kuwa na sisi (Waislamu) pia ni walipa kodi”.

Akitoa mfano zaidi Shekh Kondo alisema “Waislamu tulidai Mahakama ya Kadhi kwa miaka mingi,CCM ikaahidi ikiingia madarakani katika uchaguzi uliopita itarudisha Mahakama ya Kadhi,Maaskofu na mapadri wakaipinga (japo wao haiwahusu) lakini Serikali hii ikafyata mkia na hawajaitekeleza ahadi hiyo zaidi ya kuwasumbua na kuwafanya Masheikh wetu kama watoto wadogo.Mbali ya hayo Waislamu tumedai kujiunga na OIC waziri wa nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bwana Bernad Membe akaliambia Bunge kwamba Wizara yake imefanya utafiti kwa nchi nyingi imeona kujiunga katika OIC kutainufaisha Tanzania na hakuna madhara yoyote,lakini maaskofu walipokataa na Serikali nayo kupitia Bunge wakaondosha muswada huo Bungeni,sasa kwa nini sisi Waislamu tuendelee kuikumbatia CCM? kwa taarifa yenu,Wakristo wote wameikimbia CCM na wamejiunga na chcma chao,nanyi waislamu ondokeni CCM,chama cha kujiunga mnakijuwa”alisema bila ya kufafanua.

Aliendelea kusema “ndugu zangu Waislamu hakuna haja ya kung’ang’ania kuendelea kuongozwa na CCM kwani mzigo unapoubadili kutoka bega moja hadi bega jengine,haimaanishi unapunguza uzito,bali ni kuongeza nguvu ya kupata kasi ya kutembea zaidi,naomba harakati za mwaka 2015 tuzianze sasa”alisema Sheikh Bungo.
 HAWA NI BAADHI YA WAADHIRI WALIOHUDHURIA KONGAMANO HILO.


HAWA NI SEHEMU YA WAUMINI WA KIISLAMU