Aug 20, 2013

SHEIKH KUNDECHA ASHIKILIWA NA POLISI;



Na mwandishi wetu wa munira;
Mwenyekiti wa Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini ambaye pia ni Amir wa Shura ya Maimamu Sheikh Yusuf Kundecha amekamatwa na jeshi la Polisi .


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza Kuu Sheikh Ramadhan Sanze,Sheikh Kundecha amekamatwa na Jeshi la Jolisi Makao Makuu leo saa tatu Asubuhi baada ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano.

"Ni kweli amekamatwa,kwani aliitwa na Jeshi la polisi makao makuu majira ya saa tatu Asubuhi na mpaka muda huu ameshikiliwa na Polisi,nafikiri itakuwa ni Issue (suala) ya Sheikh Ponda",alisema Sheikh Sanze.

Wakati munira blog ikiwa inajiandaa kurusha habari hizi Usiku huu,kuna taarifa zilizotufikia kwamba Sheikh Kundecha kapata dhamana majira ya saa moja usiku huu.

Blog hii itafuatilia na kuwafahamisha kilichojiri biidhniLLAAH.