Aug 21, 2013

HABARI ZA KITAIFA;Chama cha Muslim Brotherhood chateua kiongozi mpya


 MAHMOUD EZZAT
  • MAHAKAMA KUU IMEMUACHIA HURU HOSSEN MUBARAAK.

(GMT+08:00) 2013-08-21 19:39:34
Chama cha Muslim Brotherhood cha Misri kimemteua Mahmoud Ezzat kuwa kiongozi mpya wa muda wa kundi hilo baada ya serikali ya nchi hiyo kumkamata kiongozi mkuu wa kundi hilo, Mohamed Badie. 


Wataalam wanasema, ingawa wafuasi wa chama hicho wanakamatwa au wanajificha, kukamatwa kwa Badie hakutaleta athari kubwa kuwa na madhara kwa kundi hilo, na wafuasi wenye msimamo mkali wanaweza kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi. 

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Bi. Catherine Ashton jana amemwambia waziri mkuu wa Misri kuwa yuko tayari kwenda tena nchini Misri kama atahitajika. Tayari Bi. Ashton ameshatembelea Misri mara mbili katika jitihada za kutafuta suluhisho la mgogoro unaoendelea nchini humo. 

Vurugu zinazoendelea nchini Misri zinatishia uhusiano kati ya nchi hiyo na Marekani, ambapo Baraza la juu la bunge la nchi hiyo linaweka shinikizo la kupunguza msaada unaotolewa kila mwaka nchini Misri wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.3. Msemaji wa ikulu ya Marekani John Earnest amesema, rais wa nchi hiyo Barack Obama ameitisha mkutano na timu yake ya usalama kujadili mgogoro wa Misri, na kuangalia upya msaada wa Marekani nchini Misri.

Wakati huo huo kuna taarifa zilizotufikia hivi punde kwamba mahakama kuu nchini misri imemuachia huru aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Hossen Mubaarak.