Jul 26, 2013

Waalimu Watakiwa kuwa na Umoja



Na mwandishi wa munira kutoka Kilimanjaro.

Waalimu wa madrasa nchini Tanzania wametakiwa kuwa na umoja baina yao ili kujenga heshima.


Hayo yamesemwa na DR. HUSSEN RAMADHAN MBEZI Afisa mnadhim mkuu wa Jeshi la Polisi nchi Tanzania ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano ya kuhifadhi Qur aan yaliyofanyika Himo Mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.



Amesema bila ya umoja wa kweli kwa waalimu wa madrasa,itakuwa vigumu kupata  mafanikio,



Kwa kweli ndugu zangu waalimu munafanya kazi kubwa sana,hawa watoto wamehifadhi kutokana na juhudi zenu,mimi naamini kabisa kama mutakuwa na umoja wa kweli mukafanya mambo kwa umoja,basi milango ya mafanikio ipo wazi kwenu kwa uwezo wa ALLAH S.W.”


Mapema katika hafla hiyo,mhe mgeni rasmi aliwakabidhi zawadi mbalimbali zikiwemo nishani maalumu zilitolewa kwa washindi wa mashindano hayo huku zawadi za ushindi wa Juzuu mbili zikienda kwa Madrasat Izzadin Makao makuu iliyopo Njoro Moshi Kilimanjaro.wakati zawadi ya Mshindi wa kwanza katika Juzuu moja ilienda Madrasat Tanbihul ghafilina iliyopo kijiji cha kifaru Wilaya ya Mwanga huku mshindi wa pili ikienda katika Madrasat  Izzaddin Tawfiiq wakati washindi wa nusu juzuu walitoka Madrasat Muhajirina.

 Habari hizi ni kwa mujibu wa mwakilishi wetu wa munira(Ustaadh Omar Awadh Msuya) wa Kilimanjaro.

1 comments:

  1. Enter your comment...mashallah ni jambo la kheri hilo allah awazidishie katika amali zenu njema

    ReplyDelete