Ofisi ya CUF Jimbo la Wingwi Pemba, ikiwa imechomwa moto na watu wasiojulikana. Picha na Mpiga picha Wetu
Zanzibar. Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), imeiandikia barua CUF, kuitaka
kuwasilisha majina ya mawakala watakaosimamia uchaguzi wa marudio
uliopangwa kufanyika visiwani hapa Machi 20, mwaka huu.
Mwenyekiti
wa makatibu wa CUF wa wilaya 10 za Zanzibar, Hamad Masoud Hamad ambaye
ndiye aliyeandikiwa barua hiyo na ZEC, alisema wanashindwa kuielewa
tume hiyo kwa kitendo chao cha kukitaka chama hicho na vyama vingine
vishiriki uchaguzi huo kwa madai kuwa ni batili.
0 comments:
Post a Comment