Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Misri, Ahmed Aboul Gheit ndiye
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League).
Jumuiya hiyo yenye nchi wanachama 22 imemchagua kwa kura nyingi
mwanadiplomasia huyo wa zamani wa Misri mwenye umri wa miaka 73.
Taarifa ya Arab League iliyotolewa jana Alkhamisi imesema kuwa, Aboul Gheit amechaguliwa na aghalabu ya nchi wanachama licha ya Qatar kukubali uteuzi huo shingo upande.
Nchi kadhaa za Kiarabu kama vile Algeria, Baharian, Kuwait na Libya tangu awali zilikuwa zimeunga mkono uteuzi wa Aboul Gheit, ambaye alikuwa mgombea pekee wa wadhifa huo.
Uhusiano kati ya Qatar na Misri uliingia doa baada ya jeshi la Misri kumuondoa madarakani Muhammad Morsi, rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo Julai mwaka 2013.
Gheit anakuja kuchukua nafasi ya Nabil al-Araby, ambaye mwezi uliopita alitangaza kuwa hatowania muhula mwingine wa Katibu Mkuu wa Arab League baada ya muda wake kumalizika Julai mosi.
Aboul Gheitalikuwa waziri wa mwisho wa mambo ya nje wa utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak nchini Misri ulioondolewa madaraka na wananchi mwaka 2011. Vilevile aliwahi kuwa mwakilishi wa Misri katika Umoja wa Mataifa.

0 comments:
Post a Comment