Feb 28, 2016

UMATADA WATAKIWA KUSHIRIKIANA

 
 Mwenyekiti Abdul Mswaki,akifunga mkutano mkuu.

Wanachama wa Umoja wa Maendeleo Wakaazi wa Mkoa wa Tanga waishio Dar es salaam (UMATADA), wametakiwa kushirikiana na uongozi ili kuleta maendeleo ya chama.

Nasaha hizo zimetolewa mapema leo hii na Mwenyekiti wa umoja huo Ndugu Abdul R. Mswaki wakati akifunga mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Al Haramain Jijini Dar es salaam.

Amesema njia kuu na ya msingi ni kila mwanachama kuwajibika kwa nafasi yake sambamba na kushirikiana na uongozi kwa mujibu wa katiba ambapo kupitia nyenzo hizo yatapatikana mafanikio.

"Hata shamba tulililo nalo,bila kushirikiana vyema, tusitarajie mafanikio, mwisho wa kumnukuu.



 Awali akisoma taarifa ya chama kwa kipindi cha mwezi July hadi Desemba 2015, katibu mkuu Ndugu Omar Shemzigwa alisema, UMATADA imeshaanza kulihudumia shamba hilo lenye ukubwa wa heka hamsini kwa kukata miti yote iliyokuwepo ndani ya shamba hilo,zoezi ambalo limegharimu Shilingi 2,111,500.


Kwa sasa UMATADA,inamiliki shamba lenye ukubwa wa heka hamsini lilizopo mkoa wa Tanga kwa ajili ya kilimo,na inakusudia kuanza ufugaji wa nyuki na kampuni ya ulinzi.

Aidha Umoja huo wenye wanachama Mia tatu, hadi kufikia mwezi desemba 2015 ulikuwa pesa taslimu zaidi ya Shilingi Milioni Thelethini na Nne. 



 Wanachama wa UMATADA wakifuatilia Taarifa mbalimbali kutoka kwa viongozi wao.



 

BAADHI YA WAJUMBE WAKITOA MICHANGO YAO.

0 comments:

Post a Comment