Aug 8, 2014

Watu wa tabaka la kati nchini China waishio na shinikizo wanatumia zaidi kahawa na pombe kali


Utafiti uliofanyika hivi karibuni nchini China umegundua kuwa, watu wa tabaka la kati nchini humo wananunua kahawa na pombe kali kwa wingi, na kuishi kwa shinikizo zaidi. 

Utafiti huo umeonyesha kuwa, asilimia 73.5 ya watu wa tabaka la kati nchini China wanasema wana shughuli nyingi zaidi, ikilinganishwa na kiwango cha wastani cha taifa asilimia 62.1. 

Utafiti huo umegundua kuwa, unywaji wa kahawa na vinywaji vya kuongeza nguvu kwa watu wa tabaka la kati ni asilimia 50 zaidi ya wastani wa taifa. Utafiti huo pia umegundua kuwa, watu wa tabaka hilo pia wanapendelea zaidi pombe na pombe kali kuliko watu wa matabaka mengine.

0 comments:

Post a Comment