Kutokana na ALLAH kutuwezesha kulidiriki kumi la mwisho ambalo ndani yake kuna LAYLATUL QADRI,kwa kufahamu ubora na umuhimu wa usiku huo,mkurugenzi wa munirablog ameridhia makala haya kuchapwa katika ukurasa huu,ili wasomaji wetu waweze kufaidika.
Tafadhali fuatilia makala hii.
VIPI UNAWEZA KUIPATA LAYLATUL QADRI?
Tumeingia kumi la mwisho, kumi ambalo ndani yake kuna siku
tukufu, siku ya Laylatul-Qadr, ambayo ibada yake ni bora kuliko ibada ya miezi
elfu.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala):
﴿ بِسْمِ اللّهِ
الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
((إِنَّا
أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ)) (( وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ
الْقَدْرِ)) (( لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ))
((تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ
أَمْرٍ)) ((سَلَامٌ هِيَ حَتَّى مَطْلَعِ الْفَجْرِ))
BismiLlaahir
Rahmaanir Rahiym
((Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul
Qadr, (Usiku wa Makadirio[Majaaliwa]). Na nini
kitachokujuulisha nini Laylatul Qadr?)) ((Laylatul-Qadr ni bora kuliko miezi
elfu)) ((Huteremka Malaika na Roho (Jibriyl) katika usiku huo kwa idhini ya
Mola wao kwa kila jambo)) ((Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri))
[Al-Qadr: 1-5]
Vile vile dalili katika Hadiyth
mbali mbali zimethibiti kuhusu Fadhila za usiku huu mtukufu, na jinsi Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa hali yake katika siku
hizi kumi za mwisho za Ramadhaan.
Baada ya kuzijua fadhila zake usiku huu mtukufu inakupasa Muislamu
ujikaze katika siku kumi hizi za mwisho kuacha mambo yote yanayokushughulisha
ya dunia na utumbukie katika ibada tu ili uweze kuupata usiku huo mtukufu,
yaani ukukute wewe ukiwa katika ibada ili zihesabiwe ibada zako kama kwamba umefanya ibada ya miezi elfu.
Tukifanya hesabu miezi elfu hiyo ni sawa na umri wa miaka
83!
1000 ÷ 12 = 83.3 yaani miaka
themanini na tatu na miezi mitatu takriban.
Hivyo ikiwa Laylatul-Qadr imekukuta katika ibada ya aina yoyote, ikiwa
ni Swalah (Qiyaamul-Layl), kusoma Qur-aan, kufanya aina za dhikr, kutoa sadaka,
kulisha chakula, kuwasiliana na jamaa, kujielimisha au kuelimisha, kufanya wema
kwa watu, yote hayo utaandikiwa kama umefanya hayo kwa umri wa miaka 83! Na
juu ya hivyo ibada hiyo ya usiku mmoja tu ni bora zaidi kuliko ibada
utakayoweza kufanya miaka 83 na miezi mitatu. Subhaana Allaah!
Jihadhari ndugu Muislamu usije
ukakukuta usiku huu mtukufu ukiwa katika maasi au katika sehemu ukiwa
umeghafilika na ya dunia kama sokoni, magenge ya soga au michezo ya
kupoteza wakati au kwenye televisheni ukiangalia misalsalaat, mipira na sinema
zikakupita kheri zote za usiku huu. Utaona siku hizi Waislamu wengi
wanashughulika kwenda madukani kutafuta nguo za 'Iyd khaswa kina dada wakiacha
masiku haya yawapite wakiwa humo badala ya kuwa majumbani mwao au misikitini
kufanya ibada na kutegemea kuupata usiku huu.
Ni siku chache tu ndugu Waislamu
ambazo zinakimbia kama upepo. Je, nani basi katika sisi atakayepuuza asiupate usiku huo? Na Nani
katika sisi atafanya hima kuupata usiku huo? Kwani hatujui kama tutakuweko
duniani mwakani kuzipata siku hizi au hata hatujui kama
tutaikamilisha Ramadhaan hii. Basi tujitahidi kwa kukesha siku kumi hizi
na kuamsha familia zetu ili iwe kheri yetu kukutana na usiku huo mtukufu tuweze
kupata fadhila zake hizo ambazo ni sawa na kulipwa malipo ya umri mrefu kama
tulivyoona hapo nyuma hata kama hatutoruzukiwa umri huo.
Mwenye Kuukosa Usiku Huu Amekula Khasara Kubwa
Hakika mwenye kuukosa usiku huo atakuwa amenyimwa kheri zake na itakuwa
ni khasara kuukosa usiku huu mtukufu kama
anavyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة
رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : لَمَّا حَضَرَ رَمَضَان قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى
اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (( قَدْ جَاءَكُمْ شَهْرُ رَمَضَان شَهْرٌ مُبَارَكٌ اِفْتَرَضَ
اللَّهُ عَلَيْكُمْ صِيَامَهُ تُفْتَح فِيهِ أَبْوَاب الْجَنَّة وَتُغْلَق فِيهِ
أَبْوَابُ الْجَحِيم وَتُغَلُّ فِيهِ الشَّيَاطِين فِيهِ لَيْلَة خَيْرٌ مِنْ
أَلْف شَهْر مَنْ حَرُمَ خَيْرهَا فَقَدْ حُرِمَ)) رَوَاهُ النَّسَائِيّ
Kutoka kwa Abu Huraryah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba ilipofika
Ramadhaan, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((Umekujieni mwezi wa Ramadhaan, ni mwezi wa Baraka. Imefanywa Swawm kwenu
kuwa ni Fardh, milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na
mashaytwaan hufungwa. Umo katika mwezi huu usiku ulio bora kuliko miezi
elfu. Atakayenyimwa kheri zake hakika kanyimwa haswa)) [An-Nasaaiy]
Siku hiyo ni siku iliyoteremeshwa Qur-aan kutoka mbingu ya saba hadi
mbingu ya kwanza kama Anavyosema Allaah
(Subhaanahu Wa Ta'ala):
﴿ بِسْمِ اللّهِ
الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
((حم))
((وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ)) (( إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي
لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ)) ((فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ
أَمْرٍ حَكِيمٍ))
BismiLlaahir
Rahmaanir Rahiym
((Haa
Miym)) ((Naapa kwa Kitabu kinachobainisha)) ((Hakika Tumekiteremsha katika
usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji)) ((Katika usiku huu hubainishwa
kila jambo la hikima)) [Ad-Dukhaan: 1-4]
Aya ya nne inayosema 'Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikma'
kuwa kuna makadirio ya mwaka huo na yote yatakayotokea katika mwaka mzima. Kwa
maana kwamba, siku ya Laylatul-Qadr, makadirio yote yaliyomo katika
Al-Lawhum-Mahfuudhw (Ubao uliohifadhiwa) na huteremshwa haya makadirio na
Malaika ambao wanaandika makadirio ya mwaka unaokuja yakiwa ni kuhusu umri wetu
wa kuishi, rizki zetu, na yatakayotokea yote hadi mwisho wake. [Imesimuliwa na
Ibn 'Umar, Mujaahid, Abu Maalik, Adh-Dhwahaak na wengineo katika Salaf – Ibn
Kathiyr: 8:671]
Kujikaza kufanya ibada
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa inapoingia
kumi la mwisho akijikaza kwa kufanya ibada kuliko siku zozote zingine:
عن عائشة رضي الله عنها قالت: كان رسول الله صلى الله
عليه وسلم يجتهد في العشر الأواخر ما لا يجتهد في غيره. رواه مسلم
Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba:
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijitahidi
katika kumi la mwisho kuliko alivyojitahidi katika siku nyingine zozote"
[Muslim]
Na katika
Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim):
عن عائشة رضي الله عنها، قالت: "كان رسول الله صلى الله
عليه وسلّم إذادخل العشر شذ مئزره، وأحيا ليله، وأيقظ أهله ( وفي رواية)
"أحيا الليل،وأيقظ أهله، وجدّ، وشدّ المئزر" رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwake pia Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu
'anha): "Ilipokuwa inaingia kumi (la mwisho) Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaza izaar (shuka) yake, akikesha usiku,
na akiamsha ahli zake" (Na katika riwaaya nyingine) "Akikesha usiku,
akiamsha ahli zake, akijitahidi na akikaza izaar yake"
[Al-Bukhaariy na Muslim]
Kwa Nini Umeitwa Laylatul-Qadr?
Amesema Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Llaah):
Kwanza: Kutokana na uwezo nao ni utukufu kama
vile kusema “fulani mwenye uwezo mkubwa" yaani mwenye hadhi au utukufu.
Pili: Ni usiku ambao una makadirio ya mwaka mzima na huandikwa yote
yatakayotokea mwaka huo, na hii ni Hikma ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) na
kuonyesha usanifu wa utengenezaji Wake na Uumbaji Wake.
Tatu: Usiku huo una uwezo mkubwa kama
alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
من قام ليلة القدر إيمانا
واحتسابا غفر له ما تقدم من ذنبه)) متفق عليه
((Atakayesimama usiku wa Laylatul-Qadr kwa iymaan na
kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Sababu Ya
Kupewa Waislamu Laylatul-Qadr
Sababu ya kupewa Ummah huu wetu wa Kiislamu siku hii tukufu ya
Laylatul-Qadr ni kwamba:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliona
umri wa Ummah za mwanzo ni mrefu, na umri wa Ummah wake ni mfupi
akapewa usiku wa Laylatul-Qadr uwe ni bora kuliko miezi elfu. [Muwatwtwaa 1/321
(Muhammad Fuad 'Abdul-Baaqy]
Ibada Za Kufanya Masiku Kumi Haya Katika Kukesha
1-Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku kuswali)
((من قام رمضان إيماناً واحتساباً غفر له ما تقدم من
ذنبه)) متفق عليه
((Atakayesimama (Kuswali) Ramadhaan kwa iymaan na kutaraji malipo,
ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
2-Kuosma Qur-aan
Khaswa kwa vile usiku wa Laylatul-Qadr ndio usiku ulioteremeshwa Qur-aan
kama tulivyoona katika Aayah hizo za juu
katika Suratul-Qadr na Suratud-Dukhaan.
Vile vile Ramadhaan nzima inampasa Muislamu asome Qur-aan kwani ni mwezi
ulioteremshwa Qur-aan kama Anavyosema Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala):
((شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى
لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ
الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa
watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 185]
Na Jibriyl ('Alayhis-Salaam) alikuwa akimteremkia Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) kila usiku wa Ramadhaan akimsomesha na kumsikiliza
Qur-aan:
"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ- أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ
فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ
وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ
رَمَضَانَ
فَيُدَارِسُهُ الْقُرْآنَ"- رواه
البخاري
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni
mbora (mwenye matendo mema) wa watu, na alikuwa mbora zaidi katika
Ramadhaan kwa sababu Jibriyl alikuwa akimjia kila usiku wa Ramadhaan
akimfundisha Qur-aan)) [Al-Bukhaariy]
3- I'tikaaf
Kutia nia kubakia msikitini kwa kufanya ibada tu humo kwani Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo:
عن عائشة – رضي الله عنها-
قالت "كان النبي يعتكف في كل رمضان عشرة أيام؛ فلما كان العام الذي قبض فيه اعتكف عشرين يوماً - أخرجه
البخاري
Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba:
Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya I'tikaaf
kila Ramadhaan siku kumi, ulipofika mwaka wake wa kuaga dunia alifanya I'tikaaf
siku ishirini" [Al-Bukhaariy]
4-Kuomba Maghfirah
Kwani usipoghufuriwa madhambi yako basi ni hatari!
عَنْ أَنَس وَغَيْره أَنَّ
النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا صَعِدَ الْمِنْبَر ثُمَّ
قَالَ (( آمِينَ آمِينَ آمِينَ)) " قِيلَ يَا رَسُول اللَّه عَلَامَ
مَا أَمَّنْت ؟
قَالَ (( أَتَانِي جِبْرِيل فَقَالَ يَا مُحَمَّد رَغِمَ
أَنْف رَجُل ذُكِرْت عِنْده فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيْك قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ
ثُمَّ قَالَ رَغِمَ أَنْف رَجُل دَخَلَ عَلَيْهِ شَهْر رَمَضَان ثُمَّ خَرَجَ
فَلَمْ يُغْفَر لَهُ قُلْ آمِينَ فَقُلْت آمِينَ ثُمَّ قَالَ رَغِمَ أَنْف رَجُل
أَدْرَكَ وَالِدَيْهِ أَوْ أَحَدهمَا فَلَمْ يُدْخِلَاهُ الْجَنَّة قُلْ آمِينَ
فَقُلْت آمِينَ)) صحيح الترمذي وقال الشيخ الألباني حسن
صحيح
Kutoka kwa Anas na wengineo kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) alipopanda juu ya minbar aliitikia ((Aamiyn, Aamiyn,
Aamiyn)). Alipoulizwa kwa nini ameitikia hivyo akasema: ((Amenijia Jibriyl
akasema: Ee Muhammad, ole wake yule ambaye unapotajwa hakuswalii, hivyo sema
Aamiyn. Nikasema Aamiyn. Kisha akasema: ole wake yule ambaye umeingia mwezi wa
Ramadhaan kisha akatoka bila ya kughufuriwa, kwa hiyo sema Aamiyn. Nikasema
Aamiyn. Kisha akasema: ole wake yule ambaye amewakuta wazazi wake au mmoja wa
wazazi wake lakini wasimuingize Peponi. Hivyo sema Aamiyn. Nikasema Aamiyn))
[Swahiyh At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa Hadiyth hiyo ina daraja
ya Hasan Swahiyh]
5-Du'aa Ya Kuomba Maghfirah Katika Siku
Kumi Hizi Zakaatul-Fitwr Mwisho
عن عائشة رضي الله عنها
أنها قالت يا رسول الله أرأيت إن وافقت ليلة القدر ما أدعو قال: ((تقولين:
اَللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌ تُحِبُّ الْعَفْو فَاعْفُ عَنِّي)) ابن
ماجه و صححه الألباني
Kutoka kwa mama wa waumini bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba
alisema "Ewe Mjumbe wa Allaah je, nitakapowafikiswha usiku wa
Laylatul-Qadr niombe nini?" Akasema, ((Sema: Ewe Allaah Hakika Wewe
Ndiye Mwenye Kusamehe Unapenda Kusamehe basi Nisamehe)) [Ibn Maajah na kaisahihisha
Al-Albaaniy]
Matamshi Yake
Allaahumma Innaka 'Afuwwun
Tuhibbul-'Afwa Fa'afu 'Anniy
6-Kumkumbuka Allaah Kwa Aina Zozote
Za Dhikr
Kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl,
Takbiyr (kusema: Subhaana Allaah, Alhamdulillah, Laa Ilaaha Illa
Allaah, Allaahu Akbar)
7- Kuomba Du'aa Na Haja Zako
Kwa vile ni mwezi wa kuomba Du'aa pia kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala
Ameunganisha Aayah za kufaridhishwa Swawm na Aaya za kuhusu kuomba Du'aa:
((وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ
الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُواْ لِي وَلْيُؤْمِنُواْ بِي لَعَلَّهُمْ
يَرْشُدُونَ))
((Na waja Wangu watakapokuuliza khabari Zangu, waambie kuwa Mimi nipo
karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie Mimi, na
waniamini Mimi, ili wapate kuongoka)) [Al-Baqarah: 186]
Usiku Gani
Khaswa Unapatikana Laylatul-Qadr?
Hadiyth zimetaja siku kadhaa ambazo usiku huu mtukufu hutokea katika
siku kumi za mwisho na haswa katika usiku wa witiri, zikiwa zimetajwa nyingine
kuwa ni usiku wa siku ya ishirini na moja, au ishirni na tatu, au ishirni na
tano au ishirini na saba kama ilivyokuja katika dalili zifuatazo:
وفي حديث عائشة رضي الله عنها أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((تحروا
ليلة القدر في الوتر من العشر الأواخر)) رواه البخاري
Hadiyth kutoka Mama wa Waumini 'Aiashah (Radhiya Allaahu 'anha)
kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Utafuteni
usiku wa Laylatul-Qadr katika siku za witiri kwenye siku kumi za
mwisho)) [Al-Bukhaariy]
وفي حديث ابن عباس رضي
الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((التمسوها في العشر الأواخر من
رمضان ليلة القدر في تاسعة تبقى ، في سابعة تبقى ، في خامسة تبقى)) رواه البخاري
Hadiyth kutoka Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Utafuteni usiku wa
Laylatul-Qadr katika siku kumi za mwisho za Ramadhaan, katika (usiku wa) tisa,
saba, na wa tano utakaobakia [mwisho wa Ramadhaan])) [Al-Bukhaariy]
Imaam Ahmad amerikodi kutoka kwa 'Ubaydah bin Asw-Swaamit kwamba
alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu usiku wa
Laylatul-Qadr akasema:
((فِي رَمَضَان فَالْتَمِسُوهَا فِي الْعَشْر الْأَوَاخِر
فَإِنَّهَا فِي وِتْر إِحْدَى وَعِشْرِينَ أَوْ ثَلَاث وَعِشْرِينَ أَوْ خَمْس
وَعِشْرِينَ أَوْ سَبْع وَعِشْرِينَ أَوْ تِسْع وَعِشْرِينَ أَوْ فِي آخِر
لَيْلَة))
((Katika Ramadhaan, utafuteni siku kumi za mwisho, hakika umo katika
siku za witiri, siku ya ishirini na moja, au ishirini na tatu, au ishirini na
tano, au ishirini na saba, au ishirini na tisa, au usiku wa mwisho)) [Ahmad]
Alama
Zinazobainisha Laylatul-Qadr
- Kwenye usiku huo kunakuwa na mwanga zaidi.
- Upepo siku hiyo hutulia, yaani siku hiyo hautokei upepo mkali.
- Hali ya hewa huwa nzuri.
- Nyoyo siku hizo huwa na utulivu na unyenyekevu zaidi kuliko siku nyingine.
- Baadhi ya watu wema huoteshwa usiku kama walivyokuwa wakioteshwa Maswahaba na Salafus-Swaalih (wema waliotangulia)
Asubuhi
Yake
حديث أبي بن كعب رضي الله
عنه أنه قال: "أخبرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم أنها تطلع يومئذ ٍ لا
شعاع لها" رواه مسلم
Hadiyth kutoka kwa Ubay bin Ka'ab (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba:
"Ametuambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa jua
hutoka siku hiyo likiwa halina mishale (mikali)" [Muslim]
(( ليلة القدر ليلة طلقة لا حارة ولا باردة ، تُصبح الشمس
يومها حمراء ضعيفة)) صحيح ابن خزيمة
((Laylatul-Qadr usiku ulio katika hali ya ukunjufu, usio na baridi wala
joto, asubuhi yake jua huwa jekundu na dhaifu)) [Swahiyh Ibn Khuzaymah]
ليلة القدر ليلة بلجة
(أي مضيئة) لا حارة ولا باردة ، لا يرمى فيها بنجم)) (أي لا ترسل فيها
الشهب) رواه الطبراني ومسند أحمد
((Laylatul-Qadr usiku wa kung'aa [yaani wenye mwanga] sio joto wala
baridi, na vimondo (nyota za kufyatuliwa) hazitotumwa)) [At-Twabaraaniy na
Ahmad]
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Atuwezeshe kukesha masiku haya kumi ili tujaaliwe kuupata usiku huu
mtukufu tutoke katika Ramadhaan hii tukiwa tumeghufuriwa madhambi yetu yote na
tumepewa fadhila za usiku huu mtukufu zinazolingana na kuongezewa umri wa miaka
83. Aamiyn