Mufti Mkuu wa Misri amepinga hukumu ya kifo iliyotolewa na
mahakama ya nchi hiyo dhidi ya kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin
Muhammad Badie na maafisa wengine 13 waandamizi wa harakati hiyo.
Mufti Mkuu wa Misri Shawki Allam amesema ushahidi uliotolewa dhidi ya Muhammad Badie na watuhumiwa wengine hauna hoja madhubuti za kuwatia hatiani.
Ripoti ya Mufti Mkuu wa Misri imesema ushahidi pekee uliotajwa katika hukumu hiyo ni maelezo yaliyotolewa na afisa usalama wa taifa ambayo hayakuungwa mkono na chombo kingine.
Tarehe 19 Juni Mahakama ya Jinai ya Misri ilimhukumu kifo kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimina Muhammad Badie na maafisa wengine 13 wa harakati hiyo kwa tuhuma za mauaji ya watu, uchochezi na kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Mahakama ya Jinai ya Misri inalazimika kupata maoni ya Mufti Mkuu wa nchi hiyo kabla ya utekelezaji wa hukumu ya kifo japokuwa maoni ya kiongozi huyo wa juu kabisa wa kidini hayazuii kutekelezwa hukumu za kifo za mahakama hiyo.
Hukumu ya mwisho ya mahakama hiyo itatolewa tarehe 30 mwezi huu wa Agosti.

0 comments:
Post a Comment