Aug 8, 2014

CAR kuunda mahakama maalumu ya jinai

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itaunda mahakama maalumu itakayochunguza jinai zilizofanyika katika nchi hiyo iliyoathiriwa na vita vya ndani.

Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Ghislain Grésenguet amesema kuwa mahakama hiyo maalumu itachunguza na kutathmini jinai zilizofanyika nchini humo katika vita vya ndani.

 Amesema kamati ya wanasheria 8 inapitia nyaraka za awali za kunzishwa mahakama hiyo na  itaanza shughuli zake wiki ijayo.

Awali Rais Catherine Samba- Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alikuwa ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake nchini Uholanzi kushughulikia faili la jinai zilizofanyika nchini humo.

Maelfu ya watu wengi wao wakiwa Waislamu wameuawa na malaki ya wengine kukimbia makazi yao katika mashambulizi ya kundi la Kikristo la Anti Balaka dhidi ya Waislamu walio wachache katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.  

0 comments:

Post a Comment