Aug 14, 2014

Marekani inaendelea na harakati zake nchini Iraq

Rais wa Marekani, Barack Obama, katikahotuba yake kuhusu hali inayojiri nchini Iraq.
Rais wa Marekani, Barack Obama, katikahotuba yake kuhusu hali inayojiri nchini Iraq.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuk Hagel amefahamisha kwamba washauri wengine 130 wa kijeshi watatumwa nchini Iraq katika mji wa ErbiL, mji mkuu wa Kurdistan kutathimini zaidi mahitaji ya watu wa kabila la Yazid waliofukuzwa hivi karibuni katika makaazi yao na wapiganaji wa kiislam wanaotaka kuunda taifa la Kiislamu.

Kulingana na taarifa ya jeshi la Marekani, washauri hao wa kijeshi watakuwa na jukumu la kupanga na kuratibu miradi ya kibinadamu kwa wananchi hao wachache wa kabila la Yazid.

Wanajeshi hao wamefikia idadi ya washauri mia tatu wa kijeshi ambao rais Barack Obama alitangaza mwezi Juni kuwatuma nchini Iraq kusaidia serikali ya Iraq kuzuia mashambulizi ya kundi la Isil lililokuwa likiendelea kuiteka miji kadhaa nchini Iraq.

katika hatuwa nyingine vikosi vya Marekani tayari vimefanya operesheni 17 tangu siku ya Ijumaa kuzuia kundi la Isil kuendelea kusonga mbele kwenye uwanja wa mapambano.

Wakati huo huo Tume ya Ulaya imeongeza kiasi cha euro milioni tano kama sehemu ya msaada kwa nchi ya Iraq na kuonya kuwa kuwafikia raia walio katika hali mbaya ndilo tatizo kubwa linalohitaji kutatuliwa kwa haraka na si msaada wa fedha.

Kwenye mkutano na wanahabari jumanne wiki hii kamishina wa misaada ya kibinadamu wa tume ya Ulaya Kristlina Georgieva amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia mamia ya wananchi wa Iraq wasio na makazi waliokwama kwenye milima ya Sinjar.

Georgieva amesema mzozo unaoendelea nchini Iraq ni tatizo kubwa linalohitaji mwitikio wa dharura ambapo tayari Ufaransa na Italia zimetoa wito wa hatua nzito kuchukuliwa kutatua mzozo huo.

0 comments:

Post a Comment