Majambazi wenye silaha juzi mchana walimpora meneja wa Kampuni ya
Ununuzi wa Korosho na Ufuta ya Olam, Jafari Mgumba takriban Sh47
milioni.
Majambazi hao walifanya tukio hilo eneo la Tabata TioT baada ya
kumfuatilia kwa nyuma kijana huyo akitokea duka la Quality Plaza
alipokwenda kuchukua fedha hizo kutoka Benki ya DTB.
Hata hivyo, baada ya kuporwa fedha hizo, Mgumba alitokomea bila kutoa
taarifa polisi, hatua iliyosababisha kuunganishwa na watuhumiwa. Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Maria Nzuki alisema mlalamikaji huyo
alishikiliwa na kuhojiwa kwa makosa mawili ili kujiridhisha kama
anahusika au hahusiki na tukio hilo.
“Alikuja na kujitambulisha kama mfanyabiashara wa kununua mazao ya
korosho na ufuta wa Kampuni ya Olam iliyopo Dar es Salaam, lakini
ikabidi tumshikilie kwa sababu ya kuchelewa kutoa taarifa polisi pamoja
na kutotumia askari kusindikiza fedha hizo, ulinzi ambao hutolewa bure,”
alisema.
“Kwa madai yake anasema alipoibiwa akakimbilia ofisini kwao kutoa taarifa halafu ndipo akaja kituoni,” alisema Kamanda Nzuki.
Tukio lilivyotokea
Tukio hilo lilitokea juzi saa 7:00 mchana jirani na Benki ya NMB, Tawi la Mandela Road.
Mwandishi wa habari alifika eneo la tukio na kukuta idadi kubwa ya watu
wakiwa na hofu baada ya majambazi hao kufyatua risasi tatu hewani.
Kabla ya majambazi hao kupiga risasi hewani, Mgumba alijaribu kupiga
kelele za “wezi, wezi,”, lakini akatishiwa bunduki na kulazimika
kunyamaza.
Kutokana na kitendo hicho, watu waliokuwa eneo hilo walitimka kujiokoa na wengine wakilala chini ya vibanda vyao.
Mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la
Ali alisema risasi zilipigwa baada ya raia huyo kupiga kelele za mwizi
0 comments:
Post a Comment