Aug 16, 2014

KIKONGWE WA MIAKA 80 AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI WILAYANI RUNGWE

DSC00207TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16.08.2014.

  • KIKONGWE WA MIAKA 80 AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI WILAYANI RUNGWE.
  • MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
  • MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUANGUKA.
  • BWENI MOJA LA SHULE YA SEKONDARI MARANATHA LATEKETEA KWA MOTO.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MATENKI – BODA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA BINADAMU KINYUME CHA SHERIA.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 KIKONGWE WA MIAKA 80 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ADAM MWANDIGA MKAZI WA KIJIJI CHA KIBISI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA MOHAMED MWAMELA AMBAYE ALIKUWA ANAISHI NAYE [MTOTO WA MDOGO WA MAREHEMU].
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIBISI, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI WA KIFAMILIA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA.
 MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE WENGINE WAWILI AMBAO HAWAKUWEPO WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA MSAKO KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. AIDHA ANATOA WITO KWA WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MPANDA BAISKELI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA TITO KIWITI (29) MKAZI WA NYENJELE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA USAJILI T. 519 AEE AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE MICHAEL KYANDO (27) MKAZI WA MAJENGO – TUNDUMA.
 AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA NYENJELE, KATA YA NDALAMBO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA SUMBAWANGA/TUNDUMA.
 CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA CHA NYENJELE. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
 KATIKA TUKIO LA TATU:
 MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FAUTELI SIMFUKWE (65) MKAZI WA IYUNGA JIJI NA MKOA ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI AMBAYO HAIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI AMEFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI HIYO KUACHA NJIA KISHA KUANGUKA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO EMANUEL SIMFUKWE (27) MKAZI WA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA AMBAYE ALIKUWA ABIRIA KWENYE PIKPIKI HIYO ALIJERUHIWA.
 AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO ENEO LA MTELEMKO MSANGAMWERU, KATA YA MBALIZI, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MAJERUHI ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
 KATIKA TUKIO LA NNE:
 BWENI MOJA LA SHULE YA SEKONDARI MARANATHA ILIYOPO KATA YA IWINDI, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA LIMETEKETEA KWA MOTO JANA MAJIRA YA SAA 17:20 JIONI.
 MWILE MWAMAHONJE (38) MKAZI WA MARANATHA IWINDI ALIGUNDUA KUUNGUA KWA BWENI MOJA LA WANAFUNZI LIITWALO ‘MANDELA A’. AIDHA KATIKA AJALI HIYO, MALI MBALIMBALI ZA WANAFUNZI KAMA VILE VITABU, MAGODORO 30, VITANDA NA SEHEMU YA JUU YA PAA LILITEKETEA KWA MOTO.
 CHANZO CHA MOTO HUO BADO KUFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA KWA MOTO PIA BADO HAIJAFAHAMIKA. MOTO ULIZIMWA KWA JITIHADA ZA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI NA WANANCHI. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI YA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO KWANI YANA MADHARA MAKUBWA NA YANA SABABISHA UHARIBIFU WA MALI.
 KATIKA MISAKO:
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SADIKI MWANDOLUMA (30) MKAZI WA MATENKI BODA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA BINADAMU KINYUME CHA SHERIA.
 MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.08.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA LUBELE, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA AKIWA ANAMSAFIRISHA DESTER TAMLATI (24) MKAZI NA RAIA WA NCHINI ETHIOPIA KINYUME CHA SHERIA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AMBAO WANAWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO,WAHAMIAJI HARAMU NA WENGINEO ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
           Imesainiwa na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Post a Comment