Maulamaa wa Kishia na Kisunni nchini Iraq wametoa mwito wa
kuundwa haraka serikali mpya yenye sura ya umoja wa kitaifa ili iwe
rahisi kupambana na makundi ya kigaidi na kitakfiri kama vile Daesh.
Kiongozi mashuhuri wa Kishia, Muqtada al-Sadr, amesema, njia ya pekee ya kuweza kukabiliana na matakfiri wa Daesh ni kuundwa haraka serikali itakayowajumuisha Wairaqi wote.
Maulamaa wa Kisunni pia wametoa mwito huo na kuapa kuisaidia serikali ya Waziri Mkuu Nouri al-Maliki katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh.
Huku hayo yakijiri, Waziri Mkuu, Nouri al-Maliki ameitisha kikao cha dharura cha bunge ili kujadili hali ya mambo nchini Iraq.
Bunge la nchi hiyo linatarajiwa kukutana Julai 1 ambapo pamoja na mambo mengine, litajadili muundo wa serikali mpya.
Waziri Mkuu wa Iraq pia ameishukuru Syria kwa kushambulia ngome za Daesh katika mpaka wa Syria na Iraq Siku ya Jumanne.
Al-Maliki amesema ingawa hakuiomba Syria ishambulie lakini msaada kama huo unakaribishwa wakati wowote.

0 comments:
Post a Comment