Sheria mpya dhidi ya ushoga inatoa adahabu ya maisha jela
Waziri wa mambo ya nje nchini
Uganda, Sam Kutesa amesema ana wasiwasi kuwa Marekani huenda ikasitisha
msaada wake kwa taifa hilo baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha
sheria dhidi ya ushoga nchini humo.
Bwana Kutesa amesema kuwa watu sharti wawe na maadili na kukubali msaada.
Balozi wa Marekani nchini Uganda Scott DeLisi, awali aliitaka serikali ya Uganda, kubatilisha sheria hiyo.
Alisema alihitaji kufafanuliwa zaidi sheria hiyo, kabla ya Marekani kujua ikiwa itaendelea na mipango yake ya misaada kwa nchi hiyo hasa miradi ya kupambana dhidi ya HIV na Ukimwi..
Sheria hiyo mpya, inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kupiga marufuku kile inachosema kusambaza vitendo vya ushoga.
0 comments:
Post a Comment