Kundi la Kikristo la Anti Balaka linaendeleza jinai dhidi ya
Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kubomoa makumi ya Misikiti
nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, kundi la Anti Balaka linafanya mikakati ya kufuta athari zote za dini tukufu ya Kiislamu na Waislamu kwa kuwauwa Waislamu na kubomoa Misikiti yao.
Taarifa hizo zimeongeza kuwa, mji mkuu wa jamhuri ya Afrika ya Kati umbao ulikuwa na Misikiti 36, hivi sasa umesalia na misikiti chini ya kumi tu, baada ya makumi ya mingine kubomolewa na wanamgabo wa Kikristo wa Anti Balaka.
Wakati wanamgambo wa Anti Balaka wakiendeleza jinai zao za kuwauwa kinyama Waislamu hata walioko ndani ya Misitkiti katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, vikosi vya askari wa kimataifa vya kulinda amani vimeshindwa kulinda maisha ya Waislamu nchini humo.
Wakati huo huo, magaidi wa kundi la Anti Balaka wamewapa Waislamu 800 waliokwenda kujisitiri ndani ya Kanisa Katoliki katika mji wa Carnot, kusini magharibi mwa nchi hiyo, amri ya kuondoka kanisani humo, kinyume chake wataliteketeza kwa moto wakiwemo ndani yake.
Hivi karibuni, gazeti la Daily Telegraph la Uingereza lilitangaza kuwa, genge la Anti Balaka limekuwa likifanya mauaji kwa kuwakatakata kwa mapanga, kuwatesa, kuwachoma moto na hata kuwapiga risasi Waislamu, huku vikosi vya kulinda amani vikishindwa kuzuia jinai hizo.

0 comments:
Post a Comment