Rais Obama ameagiza makao makuu
ya ulinzi nchini Marekani Pentagon kuandaa mipango ya kuwaondoa
wanajeshi wake wote kutoka Afghanistan ifikapo mwisho wa mwaka huu iwapo
hakutakuwepo maafikiano rasmi na Serikali ya Afghanistan.
Rais Obama alimpigia simu Rais Karzai wa Afghansitan juu ya mipango hiyo yake.
Mpango huo ambao tayari ulikuwa umekubaliwa na baadhi ya viongozi wa kikabila wa Afghanistan - unaandaa wajibu wa wanajeshi wa NATO unaoshirikisha kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afghanistan na kusaidia Serikali ya taifa hilo kukabiliana na wapiganaji wa Kitaliban.
Mkataba huo pia unawapa kinga ya kisheria wanajeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan.
Ikulu ya White House inasema kuwa hakuna uwezekano wa Karzai kutia sahihi mapatano hayo kabla ya kuondoka mamlakani Aprili mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment