Maofisa Usalama
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamemkamata mtu anayedaiwa kutoa
huduma kwa wagonjwa kinyume cha utaratiba na kwamba, amekuwa akiwatapeli
wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.
Akizungumza ofisini kwake jana, Ofisa Uhusiano wa
MNH, Aminieli Eligaesha alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Mustafa Kitano
na kwamba, amekuwa akitumia majina ya Dk Nyirabu na Koba, alikamatwa
wakati akimsaidia mgonjwa mmoja.
Eligeisha alisema Februari 22 mwaka huu walipata
taarifa kutoka kwa Hussein Haji kuwa, kuna daktari anaitwa Koba alitaka
kumtapeli Sh200,000 ili amtafutie kazi ya udereva kwenye tawi la MNH
lililopo Kahama Shinyanga.
Inadaiwa Haji alipofika Muhimbili alimpigia simu
daktari huyo, lakini aliambiwa kuwa wasingeweza kuonana kwa sababu
alikuwa ana kikao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, badala yake alimtaka
akutane na Dk Said Kiliwanga.
“Alimwambia kazi hiyo utakuwa analipwa Sh570,000
na posho kila siku Sh90,000, pia alimwambia amtumie namba yake ya
leseni,” alisema Eligaeshi.
Akisimulia jinsi alivyonusurika kutapeliwa, Haji
alidai Dk Kiliwanga (ambaye hajakamatwa) alimtaka atume fedha kwenye
M-Pesa ili waonane, kitendo alichokataa na kwenda kutoa taarifa kwa
walinzi wa hospitali hiyo.
Namna alivyonaswa
Eligaeshi alidai maofisa usalama wa hospitali hiyo
walipata taarifa za kuwapo kwa daktari aliyeonekana akiwahudumia
wagonjwa na kwenda kumkamata.
Baada ya kutiwa mbaroni, inadaiwa alipekuliwa na
kukutwa na kadi tatu za kliniki za wagonjwa wa Muhimbili, kitambulisho
cha Peter Daniel mfanyakazi wa hoteli moja Dar es Salaam, vipimo vya
kupimia ujauzito, namba nyingi za madaktari wa Muhimbili kwenye simu
yake ya mkononi na Sh167,000.
Wakati akiwa chini ya ulinzi, mmoja wa wagonjwa wake, aliyefahamika kwa jina la Hassan Madika alimpigia simu na kutakiwa kwenda sehemu aliyokuwa akihojiwa.
Mtuhumiwa alikiri kupigiwa simu na Madika.
Wakati akiwa chini ya ulinzi, mmoja wa wagonjwa wake, aliyefahamika kwa jina la Hassan Madika alimpigia simu na kutakiwa kwenda sehemu aliyokuwa akihojiwa.
Mtuhumiwa alikiri kupigiwa simu na Madika.
Kitano ajitetea
Kitano alisema kuwa alifika hospitalini hapo baada
ya Madika kumweleza kuwa alikuwa amefanyiwa operesheni wiki iliyopita
na kwamba, hawezi kusimama muda mrefu hivyo alikuwa akihitaji msaada wa
mtu wa kumpelekea faili sehemu husika.
Haji alipoulizwa na waandishi wa habari, iwapo anamfahamu Kitano alisema alikiri kutomfahamu na kwamba, hajawahi kumwona.
0 comments:
Post a Comment