Mtu mmoja kati ya
wanne waliolipukiwa na mabomu, Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja,
amefariki dunia na kuzikwa jana Visiwani Zanzibar.
Marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Abdallah Juma (32), alifariki dunia kutokana na majeraha makubwa aliyopata sehemu mbalimbali mwilini.
Marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Abdallah Juma (32), alifariki dunia kutokana na majeraha makubwa aliyopata sehemu mbalimbali mwilini.
Katibu wa Hospitali ya Mnazi Moja,
Hassan Makame alisema marehemu alifariki juzi jioni wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo.
Hassan Makame alisema marehemu alifariki juzi jioni wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo.
Alisema majeruhi, Pandu Haji Pandu aliyekatika
mguu amehamishiwa katika Chumba Maalumu (ICU) kutokana na majeraha
makubwa aliyopata.
Majeruhi mwingine ni Shaaban Khamis Ibrahim ambaye
anaendelea kupatiwa matibabu ikiwa ni pamoja na kutolewa kitu kigumu
sehemu ya kiunoni kilichosababishwa na mlipuko huo.
Makame alisema majeruhi Simai Hussein Hassan alipatiwa matibabu na kuruhusiwa baada ya hali yake kuimarika.
Akizungumza na gazeti hili katika wodi ya upasuaji
wa mifupa Hospitali ya Mnazi Mmoja, majeruhi Shaaban Khamis Ibrahim,
alisema mkasa huo ulimpata wakati alipokwenda karibu na karakana ya
uchongaji vyuma baada ya pikipiki yake kupata matatizo.
“Baada ya kazi zangu za uvuvi, niligundua pikipiki
yangu ina matatizo, nikaenda gereji kuifanyia matengenezo na nilipofika
jirani na wachonga vyuma, nikasikia mlipuko na kitu kizito kilikuja
kunipiga kiunoni,” alisema majeruhi huyo.
Alisema madaktari walimtoa chembechembe za mabaki ya vitu mwilini, ingawa anatakiwa kufanyiwa vipimo zaidi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamishna wa
Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alisema mtu mmoja anashikiliwa na
polisi kuhusiana na matukio ya milipuko yaliojitokeza katika maeneo
matatu Zanzibar.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Zanzibar, Michael
Hafidh alisema vyombo vya dola vinatakiwa kuwaeleza wananchi mhusika wa
vitendo vya hujuma dhidi ya makanisa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment