Umoja wa Mataifa umetahadharisha
kuhusu kushtadi hali mbaya ya kibinadamu katika Jamhuri ya Afrika ya
Kati na kuonya juu ya umwagaji mpya wa damu.
Hayo yanajiri huku Ufaransa
ikijipanga kurefusha muda wa kuweko wanajeshi wake nchini humo.
Shirika
la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeripoti kuwa maelfu
ya raia hasa kutoka jamii ya wachache ya Waislamu huko nchini Jamhuri
ya Afrika ya Kati wanakabiliwa na hatari kubwa ya mashambulizi.
Adrian
Edwards msemaji wa UNHCR ameeleza kuwa zaidi ya watu elfu 15 wengi wao
wakiwa ni Waislamu katika maeneo tafauti huko Jamhuri ya Afrika ya Kati
hivi sasa wamezingirwa na wanakabiliwa na vitisho vya Wakristo wenye
silaha.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa pia
ametaka kuongezwa wanajeshi wa kulinda amani wa kimataifa na kuimarishwa
ulinzi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati akisema kuwa misaada ya
kibinadamu pekee haitoshi.
0 comments:
Post a Comment