Jan 1, 2014

Ansar Beit al-Maqdis yadai kuyaripua makao ya Polisi Cairo

Kundi linalohamasishwa na nadharia za mtandao wa Al-Qaeda lenye makao yake katika rasi ya Sinai nchini Misri limedai kuhusika na mripuko wa bomu kwenye makao makuu ya polisi kaskazini mwa mji wa Cairo, uliyouwa askari15.
Shambulio hilo baya zaidi tangu kuondolewa kwa rais aliechaguliwa kidemokrasia Mohammad Mursi, lilibainisha changamoto zinazolikabili jeshi la Misri, katika kuwadhibiti wanamgambo walioko katika rasi ya Sinai, ambao wamewauwa wanajeshi na maafisa wa polisi zaidi ya 100 katika wimbi la mashmabulizi tangu kuondolewa kwa Mursi Julai 3, 2013.
"Ndugu zenu katika Ansar Beit al-Maqdis, kwa rehema za Mwenyezi Mungu walifanikiwa kuyalenga makao makuu ya polisi ya Daqhaleya," lilisema kundi hilo katika taarifa iliyowekwa kwenye mitandao ya Kiislamu, likizungumzia shambulio la Jumanne. 

Ansar beit al-Maqdis ilisema kuwa shambulio hilo lilifanywa na mrupuaji wa kujitoa mhanga alietambuliwa kama Abu Maryam.
Mwanjeshi wa Misri akilinda doria katika mpaka wa Misri na ukanda wa Gaza. Mwanjeshi wa Misri akilinda doria katika mpaka wa Misri na ukanda wa Gaza.

"Ugaidi mweusi"
Utawala wa mpito nchini Misri unadai kuwa kuna mahusiano kati ya wapiganaji wa jihadi wa rasi ya Sina na kundi la Mursi lenye msimamo wa wastani lakini wameshindwa kutoa wa madai hayo. 


Mursi na viongozi wengine wa juu wa Udugu wa Kiislamu walioko rumande kufuatia ukandamizaji dhidi ya kundi lao uliyofuatia kuangusha kwake, wanatuhumiwa kwa kula njama na makundi ya wapiganaji kufanya mashambulizi dhidi ya taifa.

Serikali ya Misri iliapa siku ya Jumanne kupambana na kile ilichokiita "ugaidi mweusi", na kusema kuwa shambulio hilo la Jumanne halitakwamisha mpango wa mpito ambao hatua yake inayofuata ni kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya ambayo imepangw akufanyika mwezi ujao wa Januari.

Ansar Beit al-Maqdis ilisema kwamba watawala wa Misri walikuwa wakipambana dhidi ya Uislamu na kumuaga damu za Waislamu wanaokandamizwa. Kundi hilo lilikielezea kituo cha polisi kama kiota cha "uasi wa dini na udhalimu." 

"Tunaendelea Mungu akipenda kupambana nao, lilisema kundi hilo katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya mtandao wa Kiislamu.

Salamu kwa wanajeshi, polisi
Kundi la Ansar Beit al-Maqdis, ambalo jina lake linamaanisha wakombozi wa Jerusalemu, lilidai huko nyuma kuhusika na jaribio la mauaji lililoshindwa dhidi ya waziri wa mambo ya ndani wa Misri mjini Cairo mwezi Septemba.


Kundi hilo limewaonya wanajeshi na maafisa wa polisi kuondoka katika vituo vyao ili kulinda dini yao na maisha yao. 

Lilisema kuwa limefanya shambulizi la Jumanne katika kujibu vita vya utawala dhalimu dhidi ya Uislamu na shariah (sheria za Kiislamu), kuendelea kumuaga damu za Waislamu na kuvunja heshima za wanawake na kina dada.
Msemaji wa jeshi al Misri Kanali Ahmed Ali. Msemaji wa jeshi al Misri Kanali Ahmed Ali.
Afisa wa wizara ya mambo ya ndani alisema wachunguzi wanaendelea kubaini utambulisho wa mripuaji wa kujitoa mhanga kupitia mabaki ya yaliyokutwa katika eneo la shambulizi, ambalo liliharibu kabisaa sehemu ya makao makuu ya polisi hiyo. 

Jeshi la Misri limetuma magari ya kivita na vifaru kuwamaliza wapiganaji katika rasi ya Sinai lakini hadi sasa wamekuwa na mafakio kidogo.

Kiongozi wake apiga chenga
Wanajeshi wawili waliuawa wiki iliyopita katika jaribio lililofeli la kumkamata kiongozi wa Ansar Beit al-Maqdis Shaidi al-Menei ambaye alifanyikiwa kuwatoroka. Lakini jeshi hilolinasema limewauwa "magaidi" 184 kaskazini mwa Sinai, ambayo inapakana na ukanda wa Gaza tangu kuondolewa kwa rais Mursi.


Mwezi Novemba, mashambulizi ya kundi la Beit al-Maqdis yalisababisha vifo vya wanajeshi 11 pale basi la wanajeshi lilipopita gari lililokuwa limetegwa jangwani kaskazini mwa Sinai. 

Shambulio la Jumanne hata hivyo liliishtuwa serikali inayoungwa mkono na jeshi kutokana na ukubwa wake na eneo lilikotokea. "Hii ndiyo aina mbaya zaidi ya ugaidi," alisema waziri mkuu Hazem al-Beblawi katika mazungumzo na waandishi wa habari baada ya shambulio hilo.

Baada ya shambulio hilo Bablawi alilitaja kundi la udugu la udugu wa Kiislamu kuwa ni kundi la kigaidi kwa mujibu wa msemaji, lakini alisita kulilaumu kundi hilo kwa kufanya shambulizi hilo. zaidi wa watu 1000, wengi wao wakiwa wafuasi wa udugu wa Kiislamu wameuawa katika mapigano ya mitaani na polisi katika ukandamizaji dhidi ya Udugu wa kiislamu tangu kuangushwa kwa Muhammad Mursi.
MOja ya njia za chini ya ardhi zilizokuwa zinatumiwa kusafirisha magendo kati ya Misri na ukanda wa Gaza. MOja ya njia za chini ya ardhi zilizokuwa zinatumiwa kusafirisha magendo kati ya Misri na ukanda wa Gaza.

Udugu huo unasema umedhamiria kufanya maandamano ya amani kushinikiza kurejeshwa madarakni kwa rais Muhammad Mursi, na unailaumu serikali iliyowekwa madarakani na jeshi kwa kuhusika na ghasia zinazoendelea kuikumba nchi hiyo.

Jeshi ladai kutibua njama ya Hamas
Wakati huo huo, jeshi la Misri lilisema siku ya Jumatano kwamba limetibua njama ya kundi la Hamas la Palestina kushambulia jengo muhimu la usalama kaskazini mwa Sinai. 


Msemaji wa jeshi la Misri Kanali Ahmed Ali alisema kuwa mwanachama wa kundi hilo alifichua njama hiyo wakati akihojiwa na jeshi.

Mwezi Oktoba, waziri mkuu wa Gaza Ismail Haniya alikanusha ripoti kwamba kundi lake lilikuwa linajihusisha katika mapigano katika rasi ya Sinai. 

 Hamas ambayo inatawala mjini Gaza ndiyo tawi la udugu wa Kiislamu nchini Palestina na uhusiano kati ya Misri na kundi hilo umeshuka kwa kiwango kikubw atangu kuangusha kwa rais Mursi.

Tangu wakati huo, jeshi la Misri limeharibu mamia ya handaki zilizokuwa zinatumiwa kusafirisha magendo chini ya mpaka na ukanda wa Gaza, ambazo zilikuwa zinatumika kwa ugavi wa chakula na vifa vya ujenzi kwa wakaazi wa ukanda huo.

0 comments:

Post a Comment