Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu mpya wa Jeshi la
Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini aliyestaafu Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza kesho Januari Mosi 2014 Kamishna Mangu
alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal
Intelligence) katika Jeshi la Polisi Tanzania .
Taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemteua pia Kamishna
Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi ambayo ni nafasi
mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi nchini.
Kabla ya uteuzi wake Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations),
Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya anaapishwa leo Desemba 31 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Jan 1, 2014
KAONDOKA SAID MWEMA KAJA ERNEST MANGU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment