Jan 4, 2014

TUKIMBILIE KUZIJENGA NYOYO ZETU BADALA YA KUJENGA NDIMI ZETU.




 VIJANA WA MADRASAT SIRAAJAN MUNIIRA CHINI YA UONGOZI WA USTAADH KOBA WAKIWA NA ZANA KAMILI KATIKA KUMSWALIA MTUME S.A.W.

Waislamu wametakiwa kufanya juhudi ya makusudi ya kuzijenga nyoyo badala ya utamaduni wa kuzijenga ndimi.

Hayo yamesemwa na Sheikh Clly comorian alipozungumza na Waislamu katika hafla iliyofanyika Madrasat Siraajan Muniira Tandale Jijini Dar es salaam jana usiku .

Amesema kuna utamaduni ulioota mizizi kwa baadhi ya Waislamu kuimarisha ndimi zao ili wakubalike mbele ya jamii, utamaduni ambao unaashiria kupotea kwa Ikhlaswi kwa waumini.


Alisema baadhi ya watu wanaangalia ni nani faswaha wa kusema au kusoma na wapo tayari kumdhrau ambaye ana matamshi mabaya au asiye na ufasaha wa kusema.

"Ndugu zangu Waislamu tujitahidi tuwe na Ikhlaswi katika kila jambo ili tupate radhi za ALLAAH S.W.bila ya hivyo tutakuwa na hali ngumu zaidi ya hali tulizo nazo sasa"

Aliendelea kusema kwamba "Waislamu tumekuwa na wakati mgumu hapa duniani,kiasi tkwamba una muomba ALLAAH lakini natija tuipatayo ni ndogo mno".

Sheikh Comoria alisema katika zama zilizo pita kutokana na Waislamu kua na Ikhlaswi kwa kuzijenga nyoyo zao,waliweza kufanya mambo makubwa na ya ajabu.

Hakusita kutoa mfano kwa baadhi ya wenye  IKHLASWI wa zama zilizopita kufikia hatua ya kuongea na kuwapa amri wanyama wakali pasipo wao kudhurika.

Katika hafla hiyo iliyopambika,masheikh mbalimbali walipata nafasi ya kuongea wakiwemo,sheikh Kizumwanda,Sheikh Walid Al had na Mzee Al Had.

0 comments:

Post a Comment