Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC)
ameanza kazi rasmi. Iyad bin Amin Madani ambaye ni raia wa Saudi Arabia
ameanza kuhudumu rasmi kama katibu mkuu wa taasisi hiyo ya Kiislamu
tangu jana Januari mosi mwaka 2014.
Katika hotuba yake kwenye hafla ya kukabidhiwa ofisi ilizofanyika mjini Jeddah, Madani sambamba na kuzishukuru nchi wanachama kwa kumuamini na kumchagua kushika wadhifa huo, amesema kuwa atajitahidi kuuhudumia Umma wa Kiislamu na kuchukua maamuzi kwa uadilifu.
Madani anayechukua nafasi ya Ekmeleddin Ihsanoglu aliyemaliza muda wake amesema kwamba, jumuiya ya OIC ina jukumu la kukabiliana na matatizo ya nchi wanachama na pia kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni, kijamii na kibinadamu kati ya nchi wanachama kwa njia tofauti.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) yenye nchi wanachama 57 ni taasisi ya pili kubwa zaidi inayoziunganisha serikali baada ya Umoja wa Mataifa.

0 comments:
Post a Comment