Wakimbizi wa Afrika huko Israel wametangaza maandamano mapya kulalamikia sera za ukandamizaji za Tel Aviv.
Taarifa ya Kituo cha Wakimbizi Waafrika (ARDC) imesema wakimbizi hao wataanza maandamano yao leo Jumapili kulalamikia sera za kibaguzi za utawala wa Israel dhidi ya wanaotafuta hifadhi.
Kwa muda wa wiki mbili sasa Waafrika wamekuwa wakiandamana huko Tel Aviv kupinga sheria mpya za kibaguzi na kidhalimu za Israel dhidi ya wakimbizi.
Kwa mujibu wa sheria hizo utawala wa Kizayuni wa Israel unaweza kuwafunga gereza wakimbizi kwa muda mrefu pasina kuwafungulia mashtaka au kuwarejesha walikotoka hata kama maisha yao yako hatarini.
Waandamanaji wanataka wakimbizi wote walio gerezani waachiliwe huru na haki zao zitambuliwe.
Kati kati ya mwezi Desemba, Tel Aviv ilifungua gereza ya kuwashikilia wakimbizi wa Kiafrika katika jangwa ya Negev.
Hivi karibuni pia ilibainika kuwa Mayahudi Waafrika wanaoishi Israel wanapewa dawa za kupanga uzazi ambazo zimeshapigwa marufuku katika nchi nyingi kutokana athari zake mbaya ikiwa ni pamoja na kusababisha kifo kwa anayezitumia.
Aidha duru zinaarifu kuwa wahajiri wa Kiafrika huko Israel si tu kuwa wanatumika kama panya wa maabara bali pia viungo vyao muhimu vya mwili kama figo huondolewa na kuuzwa bila idhini yao.

0 comments:
Post a Comment