Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitaka serikali ya Lebanon
ichunguze kifo cha Majed al-Majed ambaye alikuwa mpangaji mkuu wa hujuma
ya bomu dhidi ya ubalozi wa Iran mjini Beirut mwezi Novemba.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hussein Amir-Abdullahian amesisitiza kuhusu ulazima wa kuchunguza namna al-Majed alivyoaga dunia.
Jana Jumamosi Jeshi la Lebanon lilitoa taarifa na kusema kuwa Majed al-Majed, kiongozi wa kundi la kigaidi lenye mfungamano na mtandao wa al Qaeda ambaye alikuwa ametiwa nguvuni kwa kuhusika na mlolongo wa mashambulio nchini humo amefia katika hospitali ya kijeshi mjini Beirut.
Majed al-Majed ambaye ni raia wa Saudi Arabia alitiwa mbaroni siku ya Jumatatu iliyopita. Alikuwa kiongozi wa Brigedi za Abdullah Azzam, tawi la mtandao wa al Qaeda ambalo limekuwa likiendesha shughuli zake za kigaidi katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati.
Brigedi hiyo ya kigaidi ilikiri kuhusika na shambulizi dhidi ya ubalozi wa Iran tarehe 19 Novemba mwaka 2013 ambapo watu 25 waliuawa shahidi akiwemo mwambata wa utamaduni wa Iran mjini Beirut Hujjatul Islam Ebrahim Ansari.
Majed alikuwa katika orodha ya magaidi waliokuwa wakisakwa na nchi kadhaa duniani na alikuwa pia anaunga mkono kundi la kigaidi la al Nusra ambalo linapigana dhidi ya serikali ya Syria.

0 comments:
Post a Comment