Dec 30, 2013

Wanawake Waislamu Myanmar wabakwa na polisi

Wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar, wanakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na maafisa usalama katika vituo vya polisi nchini humo. 

Kwa mujibu wa ripoti maafisa wa usalama nchini Myanmar wamekuwa wakiwateka nyara wanawake na wasichana Waislamu wa kabila hilo sanjari na kuwapiga na kuwatukana. 


Habari zinasema kuwa, baada ya maafisa hao kuwalazimisha kutumia madawa ya kulevya huwapeleka katika vituo vya usalama na kuwabaka bila ya wao kujielewa. 

Hii ni katika hali ambayo jamii ndogo ya Waislamu nchini humo imekuwa ikinyimwa haki zake za kimsingi kutokana na serikali ya Naypyidaw kupinga kuwapa Waislamu wa jamii hiyo haki yoyote kwa madai kuwa eti sio raia wa nchi hiyo. 

Aidha kwa mara kadhaa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia vimavyofanywa na maafisa wa usalama na jeshi dhidi ya wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo.

0 comments:

Post a Comment