Baba wa
familia moja huko nchini Zimbabwe alijikuta akijitosa mtoni kupambana
na Mamba ili kuokoa maisha ya mwanae mwenye umri wa miaka 11 ambae
alikamatwa na mamba wakati wanavuka mto Nyaitengwa.
Baba huyo
ambae anajulikana kama Mr Tafadzwa Kachere na mwanae Tapiwa
walijeruhiwa vibaya na mamba huyo hapo jana na kupelekea wao kulazwa
katika hospitali ya Chitungwiza.
Tapiwa
alijeruhiwa kiasi cha mguu wake wa kushoto kukatwa, wakati mkono wa
kushoto wa Baba yake uliumizwa vibaya, Mr Kachere alisema kuwa mamba
huyo aliwashambulia wakati watoka katika bustani yake kuelekea
nyumbani.
Mzee huyo aliendelea kusema kuwa walipokuwa wanavuka mto huo
kijana wake akiwa nyuma alisikia mwanae akipiga mayowe ya kuomba msaada
na ndipo alipoamua kwenda na kupambana na mamba huyo ili aweze kumuokoa
mwanae aliyekua anaangaika baada ya kung'atwa mguu wake.
0 comments:
Post a Comment