Ifuatayo ni sehemu ndogo sana ya unyama uliofanywa na askari katika oparesheni ya tokomeza ujangili kama ina vyoelezwa na mwenyekiti wa kamati mhe limbeni.
Lembeli alisema ulibainika unyama mkubwa ikiwemo viongozi, madiwani,
wenyeviti wa vijiji na vitongoji na watumishi wa serikali walikamatwa na
kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza.
“Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya
wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za
siri bila ridhaa yao,” alisema.
Alisema Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai
kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa
viboko huku mwanae wa kiume akishuhudia.
“Pia alidai kulazimishwa kuchora picha ya chatu kwa kutumia wembe
kwenye paja lake.
Vilevile, Neema Moses wa Babati alidai kuvuliwa nguo
na kulazimishwa afanye mapenzi na wakwe zake na pia kuingizwa chupa
sehemu zake za siri.
“Baadhi ya akina mama walidai kubakwa na kulawitiwa.
Mfano; katika
Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na askari
wawili wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku.
“Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo wilayani Bariadi,
alibakwa na askari watatu wa Operesheni Tokomeza Ujangili huku akiwa
ameshikiwa mtutu wa bunduki,” alisema.
Alibainisha kuwa baadhi ya watuhumiwa waliopelekwa katika kambi za
mahojiano walidai kuteswa na kupewa adhabu zinazokiuka haki za binadamu
ikiwemo kuvuliwa nguo zote.
“Mfano Diwani wa Kata ya Sakasaka Wilaya ya Meatu, Peter Samwel,
alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama
kuning’inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa
kufanya mapenzi na mti,” alisema.
Aliongeza kuwa kutokana na ukatili mkubwa, baadhi ya kambi za
mahojiano zilipewa majina ya Guantanamo (Ruaha), Goligota (Ngorongoro),
Duma na Andajega (Serengeti).
Aliongeza kuwa pia operesheni hiyo iliongozwa kwa rushwa ambako
wananchi walidai kukithiri kwa vitendo vya rushwa kwa watumishi
wanaosimamia mapori ya akiba ya Maswa, Kigosi, Moyowosi, Burigi, Kimisi
na Mkungunero.
Dec 21, 2013
UFAHAMU UNYAMA ULIOFANYWA KATIKA OPARASHENI YA TOKOMEZA UJANGILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment