Dec 10, 2013

OIC yawataka walimwengu waunge mkono Palestina


Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeitaka jamii ya kimataifa iunge mkono suala la kuundwa nchi huru ya Palestina. 

Wito huo umetolewa na Mahmoud Ali Youssef, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Djibouti wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa OIC nchini Guinea Conakry. Mahmoud Ali Youssef ambaye nchi yake imekamilisha duru ya uwenyekiti wa mzunguko wa OIC amesema kuwa, kadhia ya Palestina ndiyo maudhui muhimu kwa jumuiya hiyo.
Amesisitiza kwamba, jamii ya kimataifa inapaswa kuuunga mkono juhudi za Wapalestina za kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul Muqaddas.  

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Djibouti  ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za maana na za kivitendo kwa shabaha ya kukomesha uvamizi na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Kikao cha siku tatu cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kilianza jana mjini Conakry, Guinea ambapo kadhia ya Palestina ni miongoni mwa ajenda kuu za mkutano huo.

0 comments:

Post a Comment