Khatibu wa Masjidul Aqswa Palestina
amelaani vikali mipango ya Marekani kuhusiana na mazungumzo eti ya amani
kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala haramu wa Israel.
Sheikh Akramah Sabri amesema kuwa, mipango inayopendekezwa na Marekani
kwa ajili ya mazungumzo ya mapatano kati ya Mamlaka ya Ndani ya
Palestina na Israel inalenga kupora ardhi za Wapalestina na kujengwa
vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi.
Khatibu wa Masjidul Aqswa ameweka wazi
kwa kusema kwamba, mapendekezo ya John Kerry, Waziri wa Mashauri ya
Kigeni wa Marekani hayana natija na ni mapendekezo ambayo hayana faida
yoyote kwa wananchi madhulumu wa Palestina.
Amesema, taifa la Palestina
katu halikubali mapendekezo kama hayo kwani ni ufumbuzi wa kadhia ya
Palestina kupitia njia za haramu na batili. Wakati huo huo, Khalid
Mash'al,
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu
ya Palestina HAMAS, amemtaka Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya
Palestina kuacha kufanya mazungumzo na utawala wa Kizayuni wa Israel
akisema kuwa, mazungumzo hayo hayana faida yoyote.
0 comments:
Post a Comment