Msemaji wa tume ya utetezi wa aliyekuwa rais wa Misri Muhammad
Mursi na kiongozi wa Ikhwanull Muslimin katika faili la matukio ya ikulu
ya Ittihaadiyyah nchini humo, ametangaza kuwa, leo tume hiyo
itawasilisha ombi lake rasmi la kutaka kuainishiwa muda wa kukutana na
mteja wao huyo.
Muhammad Ad-Damati amesema kuwa, lazima tume hiyo ikutane na rais huyo aliyeuzuliwa madarakani na jeshi la nchi hiyo kabla ya tarehe ya kufikishwa kwake mahakamani.
Mursi anatuhumiwa kuhusika katika matukio ya ikulu ya Ittihaadiyyah yaliyopelekea kuuliwa watu watatu kati ya waandamanaji na halikadhalika kufanya ujasusi kwa ajili ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na hadi sasa anaendelea kushikiliwa na jeshi la nchi hiyo katika jela ya Burj al-Arab ya mkoa wa Alexandria nchini humo.
Aidha rais huyo wa zamani wa Misri anatarajiwa kupandishwa kizimbani, mnamo tarehe 8 Januari mwakani.
Hayo yanajiri katika hali ambayo hali ya machafuko bado vinaendelea kushuhudiwa nchini Misri ambapo hapo jana machafuko na uchomaji moto vilishuhudiwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar kati ya jeshi na wanafunzi wanaomuunga mkono Mursi.
Mbali na hapo pia jana watu watano waliripotiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka kati ya askari usalama na wafuasi wa Muhammad Mursi Rais halali wa nchi hiyo aliyepinduliwa na jeshi mwezi Julai mwaka huu.

0 comments:
Post a Comment