SHEIKH MUHARRAM KIZUWANDA.
Waislamu wamekumbushwa kwamba kamwe hawawezi kuwa wapenzi wa kweli wa Mtume MUHAMMAD S.A.W. kama hawa watazami kwa wema Waalimu wanaofundisha QUR AAN,
Ujumbe huo umetolewa usiku wa kumkia leo katika viwanja vya Madrasat Tadhwammun iliyopo Magomeni mapipa Jijini Dar es salaam.
Akiwa ni mmoja miongoni mwa Masheikh waliopata fursa ya kuongea na mamia ya Waislamu waliofurika katika hafla ya Maulid Nabii S.A.W. Sheikh Muharram Kizuwanda alisema ufike wakati Waislamu wampende Mtume S.A.W. ki kweli.
Akimtolea mfano Swahaba Abuo bakri R,A, Sheikh Kizuwanda alisema,Swahaba huyu alimpenda sana Mtume S.A.W kwa nafsi yake na kwa mali zake zote hadi ALLAH akamtaja katika Qur aan Suratu Llayl Aya ya 19-21.
"Ndugu zangu napenda niwakumbushe kitu muhimu,Tarehe 12/09/622 Saa sita mchana,wakati Mtume S,A,W, anatoka makkah na kuhamia madina alifuatana na Sayyidna Abuobakr,kutokana na umbali mrefu Sayyidna Abuu bakr ilifikia khatua akambeba Mtume S.A.W mabegani mwake baada ya kumuona Mtume S.A.W.amechoka"Alisema.
Aliendelea kusema kwamba "hata pale ilipobidi waingie katika Jabal Thawr ili wajifiche,Abuo bakar R.A.alimzuwia Mtume asiingie kwanza,ili atangulie Abuobakr na kama kuna madhara yamkute yeye Abuobakr na si Mtume ".
Watu wakiwa wametulizana kumsikiliza aliendelea"Sayyidna Abuo bakr alilisafisha Jabali lote lenye kiza na hata Mtume S.A.W. alipoingia,Abuobakri kwa Ridhaa yake alimlaza Mtume S.A.W.mapajani kwake ili apumzike,haya ndiyo mapenzi ya kweli".
"Ndugu zangu,kitu muhimu ni kwamba mapenzi yetu kwa Mtume S.A.W hayawezi kuwa ya kweli kama hatutowatazama kwa wema Waalimu wa Qur aan,kwani bila ya Waalimu wa Quraan hata haya Maulid tusingesoma".
Alizidi kusema"Inasikitisha kuona kwamba licha ya kazi ngumu na kubwa inayofanywa na waalimu wa Qur aan,lakini ndio wamekuwa na maisha magumu zaidi huku Waislamu wenye uwezo wakibadilisha Magari kila kukicha".
Katika hafla hiyo iliyotanguliwa na Maulid ya akina mama yaliyofanyika mchana,Madrasa na Masheikh mbalimbali wandani na nje ya nchi walihudhuria.
Madrasat Tadhwammun ilianzishwa mwaka 1985 chini ya Sheikh Ahad,na imefanikiwa kutoa wanafunzi,waalimu,maimamu na makhatwibu wengi hapa nchini.
SHEIKH AL HAD,KIONGOZI MKUU WA MADRASAT TADHWAMMUN.
BAADHI YA WAUMINI WALIFURIKA KATAIKA HADHARA HIYO.
USTAADH KOBA AKIWAONGOZA VIJANA WAKE KATIKA KUMSWALIA MTUME S.A.W.
0 comments:
Post a Comment