Nov 27, 2013

UN imeshindwa kutatua kadhia ya Palestina'


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amesema kuwa, kuendelea kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kunakofanywa na utawala katili wa Kizayuni, kunaonyesha kushindwa jamii ya kimataifa katika kutatua kadhia hiyo.


Nabil al Arabi ameyasema hayo leo na kuongeza kuwa, kuendelea kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kulikoanza tangu miongo sita iliyopita, kunaonyesha wazi kushindwa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo katika kutekeleza hati ya kutatua kadhia hiyo.

 Al Arabi ameongeza kuwa, kwa kipindi chote cha miongo sita, wananchi wa Palestina wamevumilia kwa kiasi kikubwa kila aina ya mateso yanayotokana na uvamizi wa ardhi zao na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, suala ambalo halina mfano wake hata mmoja katika historia yote ya mwanadamu. 

Aidha amesema, jinai zinazotendwa na utawala katili wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, zinaufanya utawala huo kushika nafasi ya kwanza katika kukiuka sheria za kimataifa duniani.

0 comments:

Post a Comment