JESHI la Polisi Kikosi cha Wanamaji Bandarini Tanzania limesema
litakichukulia hatua za kisheria chombo cha habari kilichoripoti habari
kuhusu wizi wa kontena la kompyuta za Rais, Paul Kagame wa Rwanda.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi
ambaye ni Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji Bandari, Mboje Kanga alisema
jeshi hilo limesikitishwa na habari iliyotolewa na chombo hicho kuwa
watuhumiwa wa tukio hilo hawajakamatwa.
Alisema taarifa za chombo hicho zinadai kuwa jalada hilo limekaliwa
na watuhumiwa hawajakamatwa, jambo ambalo si kweli watuhumiwa wanne
wamekamatwa na kesi hiyo ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke na
kusajiliwa kwa namba 499/2012 na ipo katika hatua ya usikilizwaji na
itasilikizwa tena, Novemba 18 mwaka huu.
Hata hivyo, alisema chombo hicho kilidai kuna madini ya shaba
yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchini
Zambia yaliibiwa, ambapo ukweli ni kwamba madini hayo yalikuwa yanatokea
Zambia na yalikuwa katika bandari hiyo ili yasafirishwe kwenda ng’ambo.
Pia alisema uchunguzi ulifanyika na watuhumiwa wanane walikamatwa na
kesi iko Mahakama ya Wilaya ya Temeke na kusajiliwa namba 752/2012 na
ipo katika hatua ya usikilizwaji, ambapo itasikilizwa, Novemba 19 mwaka
huu.
Alisema tukio la wizi wa mafuta bandarini ni la kweli na liliripotiwa
kituo cha Polisi Kilwa Road, uchunguzi ulifanyika na watuhumiwa wanne
walikamatwa na kufikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Temeke na
kusajiliwa kwa namba 747/2012 na ipo katika hatua ya usikilizwaji.
Nov 15, 2013
Polisi Kukiadabisha Chombo Cha Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment