Assalaamu ‘Alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh
Tunapenda kuwakumbusha kuhusu Swawm ya ‘Aashuraa ambayo itakuwa Alkhamiys 10 Muharram 1435H (14 Novemba 2013M).
Ni vizuri mtu kufunga siku ya kabla
yake vilevile ambayo ni Jumatano 9 Muharram na asipojaaliwa basi anaweza
kufunga na siku ya baada yake ambayo ni Ijumaa 11 Muharram, na ikiwa
ameshindwa basi muhimu hiyo siku ya Alkhamiys10 Muharram ajitahidi
asiikose.
09 Muharram 1435H = Jumatano 13 Novemba 2013M.
10 Muharram 1435H = Alkhamiys 14 Novemba 2013M.
Fadhila Za Swawm Ya ‘Aashuraa
قال النبي صلى الله عليه وسلم : ( صيام يوم عاشوراء ، إني أحتسب على الله أن يكفر السنة التي قبله) رواه مسلم
Kasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi
wa aalihi wa sallam): (Funga ya siku ya 'Aashuraa, nataraji kutoka kwa
Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia) [Muslim]Fadhila Za Mwezi Huu Khaswa
Ingawa miezi minne yote iliyotajwa katika Aayah ya juu ni mitukufu lakini mwezi huu wa Muharram umefadhilishwa zaidi ya miezi mingine kama ilivyo katika Hadiyth zifuatazo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ ) رواه مسلم
عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا
قَالَ : "مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ
يَتَحَرَّى صِيَامَ يَوْمٍ فَضَّلَهُ عَلَى غَيْرِهِ إِلّا هَذَا الْيَوْمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَهَذَا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَنِان "رواه البخاري
Swawm ya 'Aashuraa imependezeshwa hata kwa watoto kuifunga kama walivyokuwa wakifanya Maswahaba katika siku hiyo.
عن الرُّبيّع بنت معوذ رضي الله عنها قالت: "أرسل رسول الله صلى الله عليه وسلم غداة عاشوراء إلى قرى الأنصار "من أصبح مفطرا فليتم بقية يومه ومن أصبح صائما فليصم" ، قالت : فكنا نصومه بعد ونصوّمه صبياننا ... رواه البخاري ومسلم
Akasema (Ar-Rubay'i: 'Tulikuwa tukifunga baada yake na tukiwafungisha watoto wetu...' [Al-Bukhaariy na Muslim]
Sababu Ya Kufunga Siku Ya 'Aashuraa
عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: " قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ فَرَأَى الْيَهُودَ تَصُومُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَقَالَ: (مَا هَذَا) قَالُوا هَذَا يَوْمٌ صَالِحٌ هَذَا يَوْمٌ
نَجَّى اللَّهُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ عَدُوِّهِمْ فَصَامَهُ مُوسَى،
قَالَ: ( فَأَنَا أَحَقُّ بِمُوسَى مِنْكُمْ) فَصَامَهُ وَأَمَرَ
بِصِيَامِهِ" رواه البخاري
Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): (Mimi nina haki zaidi juu ya Muwsaa kuliko nyinyi).
Akafunga siku hiyo na akaamrisha ifungwe" [Al-Bukhaariy]
Lakini Mtume wetu (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha kuwa tukhitilafiane na Mayahudi kufunga siku hiyo kwa kuongeza siku moja kabla.
روى عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قال : "حِينَ صَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ يَوْمٌ تُعَظِّمُهُ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (فَإِذَا كَانَ الْعَامُ الْمُقْبِلُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ صُمْنَا الْيَوْمَ التَّاسِعَ) قَالَ فَلَمْ يَأْتِ الْعَامُ الْمُقْبِلُ حَتَّى تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ". رواه مسلم
Akasema (Ibn 'Abbaas) haukufika mwaka uliofuata ila alifariki Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Muslim]
Kwa hiyo ni bora kufunga siku ya tisa na kumi Muharram, na kama mtu hakujaaliwa kufunga siku ya tisa na kumi, basi afunge siku ya kumi na kumi na moja.
Na kama mtu hakujaaliwa kufunga hivyo basi afunge siku ya kumi peke yake ili asikose kupata fadhila ya siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment