Nov 8, 2013

UWANJA WA MAARIFA;IJUWE ASILI YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU


Miaka yetu ya Kiislam imeanza kuhesabika baada ya kuhama (Hijrah) kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba kutoka Makkah kuhamia Madiynah. 

Baada ya kuhama, 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) akatoa shauri kuwa kwa vile ni mara ya mwanzo wanahamia katika mji ambao wataanza kutumia Sharia'h ya Kiislam, basi ni bora kuanza kuhesabu miaka kwa kuanzia mwezi huo waliohama, nao ni mwezi uliojulikana kama Muharram. 

Na pia inasemekana kuwa 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa akipata barua kutoka kwa mabalozi wake wa nchi mbalimbali zilizokuwa chini ya Uislam, na zilikuwa zikiandikwa majina ya miezi bila tarehe. 

Akawashauri Maswahaba wenzake kuwa kuwe na tarehe. 

Wako waliopendekeza tarehe zianze kwa kufuata miaka ya kirumi, na wako waliopendekeza zianze kwa miaka ya kifursi.

 Mwishowe wakakubaliana ianze pale alipohamia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah.

 

Na mwaka huu wa Kiislam ambao unafupishwa kama A.H (After Hijrah) au H kwa kirefu yenye maana  Hijriyahau , tarehe 1 Muharram A.H ilikuwa ni sawa na tarehe 16 Julai 622M. 


Yafuatayo ni majina ya miezi ya Kiarabu;
MUHARRAM;              mwezi wa kwanza.
SWAFAR;                    Mwezi wa pili.
RABIIL AWWAL;          mwezi wa tatu.
RABII THAN;               mwezi wa nne.
JAMADUL AWWAL;     mwezi wa tano.
JAMADUL AKHIR;       mwezi wa sita.
RAJAB;                       mwezi wa saba.
SHAABAN;                  mwezi wa nane.
RAMADHAN;               mwezi wa tisa.
SHAWWAL;                 mwezi wa kumi.
DHUL QAADAH;          mwezi wa kumi na moja.
DHUL HIJJAH;             mwezi wa kumi na mbili.
 

 

0 comments:

Post a Comment