(إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللّهِ يَوْمَ خَلَق السَّمَاوَات وَالأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ فَلاَ تَظْلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ)
Tafsir;Idadi
ya miezi (ya mwaka mmoja) mbele ya Allaah ni miezi kumi na mbili katika
ilimu ya Allaah (Mwenyewe tangu) siku Alipoumba mbingu na ardhi. Katika
hiyo imo minne iliyo mitukufu kabisa (nayo ni Rajab, Dhul-Qa'adah,
Dhul-Hijjah na Muharram) (kufanya) hivi ndiyo dini iliyo sawa. Basi
msijidhulumu nafsi zenu (kwa kufanya maasi) katika (miezi) hiyo)) [At-Tawbah 9:36]
Na Mtume (S.A.W) amesema katika Hadiyth iliyotoka kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu 'anhu):
(السنة اثنا عشر شهرا، منها أربعة حرم: ثلاث متواليات، ذو القعدة، وذو الحجة، والمحرم، ورجب مضر الذي بين جمادى وشعبان)) رواه البخاري، ومسلم
(Mwaka
una miezi kumi na mbili, minne miongoni ya hiyo ni mitukufu, mitatu
inafuatana pamoja; Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Muharram na Rajab ambao
uko baina ya (mwezi wa) Jumaada na Sha'abaan) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Ni
neema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kutujuaalia kuwa na
miezi iliyo bora kuliko miezi mingine au masiku bora au masaa bora
kuliko mengine, ambazo thawabu za mema yanayotendeka humo huwa ni zaidi
ya nyakati nyingine.
Ingawa
miezi minne yote iliyotajwa katika Aayah ya juu ni mitukufu lakini
mwezi huu wa Muharram umefadhilishwa zaidi ya miezi mingine kama ilivyo katika Hadiyth zifuatazo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ ) رواه مسلم
Imepokelewa
na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kasema; Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Funga bora kabisa baada ya
Ramadhaan ni funga ya mwezi wa Allaah wa Muharram)) [Muslim]
عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا
قَالَ : "مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ
يَتَحَرَّى صِيَامَ يَوْمٍ فَضَّلَهُ عَلَى غَيْرِهِ إِلّا هَذَا الْيَوْمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَهَذَا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَنِان " رواه البخاري
Imepokelewa
na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Sijapata
kumuona Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisubiri
kufunga siku yoyote kama siku hii ya siku ya 'Aashuraa na mwezi huu yaani mwezi wa Ramadhaan" [Al-Bukhaariy]
Swawm ya 'Ashuraa imependezeshwa hata kwa watoto kuifunga kama walivyokuwa wakifanya Maswahaba katika siku hiyo.
عن الرُّبيّع بنت معوذ رضي الله عنها قالت: "أرسل رسول الله صلى الله عليه وسلم غداة عاشوراء إلى قرى الأنصار "من أصبح مفطرا فليتم بقية يومه ومن أصبح صائما فليصم" ، قالت : فكنا نصومه بعد ونصوّمه صبياننا ... رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwa Ar-Rubay'i bint Mu'awwadh (Radhiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma ujumbe Alfajiri ya siku ya 'Ashuraa katika vijiji vya Answaar "Aliyeamka
akiwa amefuturu amalize siku yake (kwa kutokula) na aliyeamka amefunga
afunge" Akasema (Ar-Rubay'i: 'Tulikuwa tukifunga baada yake na
tukiwafungisha watoto wetu...' [Al-Bukhaariy na Muslim]
Ndugu
Waislam, hii ni fursa kubwa ya kujisafisha na dhambi na kuzidisha taqwa
(ucha Mungu) ili kujibebea zawadi nyingi twende nazo Akhera kwa vile
hatujui amali njema zipi zitakazokubaliwa na Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) na hatujijui kama tutakuwa na umri wa kuchuma zaidi.
SABABU ZA KUFUNGA ZA MUHARRAM;
عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: " قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ فَرَأَى الْيَهُودَ تَصُومُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَقَالَ: (مَا هَذَا) قَالُوا هَذَا يَوْمٌ صَالِحٌ هَذَا يَوْمٌ
نَجَّى اللَّهُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ عَدُوِّهِمْ فَصَامَهُ مُوسَى،
قَالَ: ( فَأَنَا أَحَقُّ بِمُوسَى مِنْكُمْ) فَصَامَهُ وَأَمَرَ
بِصِيَامِهِ" رواه البخاري
Imepokelewa
na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema "Alielekea Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah akawaona Mayahudi
wanafunga siku ya 'Aashuraa, akasema: (Nini hii?) (yaani kwa nini
mnafunga?) Wakasema hii ni siku njema, hii ni siku Allaah Aliyowaokoa
Wana wa Israili kutokana na adui wao, na Muusa alifunga siku hii.
Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): (Mimi nina
haki zaidi juu ya Muusa kuliko nyinyi). Akafunga siku hiyo na
akaamrisha ifungwe" [Al-Bukhaariy]
Lakini
Mtume wetu (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha
kuwa tukhitilafiane na Mayahudi kufunga siku hiyo kwa kuongeza siku moja
kabla.
روى عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قال : "حِينَ صَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ يَوْمٌ تُعَظِّمُهُ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (فَإِذَا كَانَ الْعَامُ الْمُقْبِلُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ صُمْنَا الْيَوْمَ التَّاسِعَ) قَالَ فَلَمْ يَأْتِ الْعَامُ الْمُقْبِلُ حَتَّى تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ". رواه مسلم
Imepokelewa
na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema "Alipofunga Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya 'Aashuraa na
akaamrisha ifungwe wakasema: Ewe Mtume wa Allaah, hii ni siku
wanayoitukuza Mayahudi na Manaswara. Akasema Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam): (Ikifika mwakani In shaa Allaah tutafunga
siku ya tisa pia). Akasema (Ibn 'Abbaas) haukufika mwaka uliofuata ila
alifariki Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Muslim]
Kwa
hiyo ni bora kufunga siku ya tisa na kumi Muharram, na kama mtu
hakujaaliwa kufunga siku ya tisa na kumi, basi afunge siku ya kumi peke
yake ili asikose kupata fadhila ya siku hiyo.
Kwa vile siku hii ni siku Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyomnusuru Muusa ('Alayhis-Salaam) na Wana wa Israaiyli,
na sisi pia tutakaofunga tuwe na tegemeo kuwa nasi Allaah (Subhaanahu
wa Ta'ala) Atatunusuru pia kutokana maadui wetu na mabaya kama Alivyotuahidi In shaa Allaah
((إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ))
(Bila
ya shaka Sisi Tunawanasuru Mitume Yetu na wale walioamini katika maisha
ya dunia ya siku watakaposimama mashahidi (kushuhudia amali za viumbe) [Ghaafir 40: 51]
Juu ya kwamba fadhila ya kufunga Swawm ni ibada Aipendayo kabisa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama ilivyo katika Hadiyth mbali mbali, vilevile funga hii itatusafisha na madhambi ya mwaka mzima,
قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( صيام يوم عاشوراء ، إني أحتسب على الله أن يكفر السنة التي قبله)) رواه مسلم
Kasema
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): (Funga ya siku
ya 'Aashuraa, nataraji kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka wa
nyuma) [Muslim]
0 comments:
Post a Comment