- MIONGONI MWAO NI WATANZANIA
WAKATI Serikali ikiendelea k u u s a k a m t a n d a o unaofanya
biashara ya dawa za kulevya nchini, Jeshi la Polisi Kitengo cha Kupambana na
Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, limekiri kuwanasa zaidi ya watu 100 waliokuwa na
dawa za kulevya na kesi zao zinaendelea mahakamani.
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha kupambana na na kuzuia Dawa za kulevya nchini kamishna Msaidizi (ASP) Godfrey Nzowa al i s ema kati ya watu hao, baadhi
yao kesi zao
zipo Mahakama Kuu.
k w a k a w a i d a
watuhumiwa wanapokamatwa na dawa hizo, hufunguliwa mbele ya mashahidi akiwepo
mtuhumiwa mwenyewe ili kuthibitisha na baadaye kupelekwa mahakamani kama
kielelezo na mahakama hupata fursa ya kuzifungua na kuziangalia kama ndizo
zenyewe.
"Wakati kesi ikiendelea, dawa hizo
huhifadhiwa ambapo kesi ikimalizika na kutolewa hukumu, ma h a k ama h u t o a
amr i y a kuteketezwa ambapo mwaka 2012, Mahakama Kuu iliteketeza kilo 92.
Kamishna Nzowa alikwenda mbali zaidi na
kuweka wazi takwimu za watuhumiwa waliokamatwa na dawa hizo kuanzia mwaka 2009
hadi Mei mwaka huu na kudai kuwa, hadi sasa zaidi ya kilo 841.3 za cocaine,
175.64 za heroine na 10.8 (bangi), zimekamatwa.
Orodha ya majina ya watuhumiwa na dawa
walizokamatwa nazo kwenye mabano ni pamoja na Steven Gwaza, (heroin gramu
825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroine gram 1,800), Khatibu Bakari Khatibu na
Khalid Salim Maunga (cocaine gramu 1,007.4).
Wengine Dhoulkefly Awadh (cocaine gramu
893.58), Abdallah Pashua Kipevu (heroine gramu 31,000), Diaka Brama Kaba
(heroin gramu 31,000), ambaye alikamatwa akiwa na wenzake Ndjane Abubakar,
Sylivia Kaaya Namirembe, Farid Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi.
Wengine ni Rashid Salim Mohamed, (cocaine
gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza (cocaine gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou
(cocaine gramu 850), Kwako Sarfo, Mnigeria (cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha
Musa (cocaine gramu 286), aliyekuwa na Aman Saidfadhil Daruweshi na Afshin
Jalal.
Jack Vuyo, (heroine gramu
42,000) huyu alikuwa na Anastazia Elizabeth
Cloete, Simon Eugenio Fadu(cocaine gramu 8,000), Assad Aziz, (heroine gramu
50,000), alikuwa na Isamil Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.
Anna Jamaniste Mboya,
(cocaine gramu 1,140), Fredy William Chonde (heroine gramu 175,000), Kambi
Zuber, Abdul Ghan na Shahbaz Malik, Livinus Malik (Wapakistani) waliokamatwa na
(cocaine gramu 804.7).Chukwudu Denis Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan
(Wanigeria) (cocaine gramu 81,000).Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo,
(cocaine gramu 1,530).
Kadiria Said Kimaro
(heroine gramu 1,365.91), Abdallah Rajab Mwalimu (cocaine gramu 716.5), Mwiteka
Godfrey Mwandemele (cocaine gramu 1,112), Abbas Kondo Gede (cocaine gramu
1,112), Mwanaidi Ramadhan Mfundo (cocaine gramu 5,000), ambaye alikuwa na Sarah
David Munuo.
Antony Karanja, Benny
Ngare, Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim, Aisha Said Kungwi, Rajab Juma
Mzome na John William Mwakalasya, Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu 97,000)
alikuwa na Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa na
Hamidu Kitwana Karimu.
Ramadhan Athuman (heroine
gramu 3,000) alikuwa na Rashid Mohammed, Ally Mohammed Kichaa na Issa
Abdulrahman.
Rashid Ally Mtopea (heroin
gramu 12,000) alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam, Maurine Amatus Lyumba,
John Adams Igwenma wa (Mnaijeria) ( cocaine gramu 830.19). Upendo Mohammed
Cheusi, Abdallah Omar Salum (cannabis sativa gramu 1,000) alikuwa na Cosmos
Chukwumezie, Ifeanyi Malven Kalu Oko (Wanaijeria) (heroin gramu 3,185.38),
Allan Duller (cocaine gramu 3,882.92), Alberto Mendes kutoka Ghana, (gramu
1,277.10 za heroine)
Wengine ni Joseph Chukwumeka Nwabunwanne
ambaye ni raia wa Nigeria, (gramu 1,245.96 za heroin) Kwaku Safo Brobbey Mghana
(gramu 13,781.78 za heroine), Princewill Ejike Mnigeria (gramu 981.12 za
heroin), Mary Mvula Mzambia (gramu 391.51 za cocaine), Waziri Shaban Mizongi,
(gramu 2,013 za heroine) akiwa na Santos Joseph Mpondela, Kelvin Kelven
Mwazeni.
Wengine ni Emmanuela Adam, Mghana (gramu
9,838.1 za cocaine), Asha Omary Ramadhan, (gramu 1.56), Mariam Mohammed Said,
(gramu 9,857.54 za bangi) akiwa na Abdullatif A. Fundikira.Aliendelea kuwataja
Marceline Koivogui, Mghana (gramu 1,073.82 za heroin), Edwin Cheleh Swen
Mliberia (gramu 1,509.35 za heroin), akiwa na Benjamin Obioma Onuorah wa
Nigeria, Sofia Seif Kingazi, (gramu 3,379.54 za cocaine) na Josephine Mumbi
Waithera Mkenya (gramu 3,249.82 za cocaine).
Iddi Juma Mfaume,(gramu 563.25 za
heroine), Amina Kassim Ramadhani,(gramu 1,980.11 za heroine) na Vivian Edigin
Mnigeria (gramu 797.56 za cocaine), Hadija Tambwe, (gramu 33,507.04 Za
cannabis), Sasha Farhan na Mnyeke Sativa, na Mychel Andriand Takahindangeng
Muindonesia, gramu 3,932.44 za cocaine).
We n g i n e n i K r i s t i n a
Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen Basil Ojiofor Mnigeri
(gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, (gramu 1,793 za heroine),
Khamis Said Bakari (gramu 1,793 za heroine).Kundi la mwisho ni Tabia Omary au
Neema Omary (gramu 994.97 za heroine), Masesa au Habiba Andrew Joseph, (gramu
1,037.9 za heroin). Hivi karibuni Agness Gerald "Masogange" na mwenzake
walikamatwa Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za dawa hizo.
Akizungumzia sakata la Mtanzania
anayedaiwa kukamatwa Mjini Dubai, Falma za Kiarabu, juzi akiwa na kilo tatu ya
dawa za kulevya aina ya cocaine, alisema yupo safarini hivyo suala hilo atalitolea ufafanuzi
leo baada ya kufika ofisini.
Dawa hizo zinadaiwa kuwa na thamani ya
Diraham milioni tatu, (sawa na sh. bilioni 1,321.7 za Kitanzania).Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo News, ambao haujataja
jina la mwanamke huyo, ulisema dawa hizo ziliwekwa kwenye mabegi na baada ya
kuhojiwa na Maofisa Usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mjini Dubai, alidai
kuwekewa dawa hizo na rafiki wa mumewe nchini Brazil (hakutajwa jina).
"Mume wangu kupitia rafiki yake,
aliamua kunitumia kama punda niweze kuyabeba mabegi haya kwa kuyarudisha
nyumbani Tanzania,"
alisema mwanamke huyo wakati akihojiwa na Ofisa mmoja wa Polisi Mjini Dubai.
Kwa mujibu wa mtandao huo, mwanamke huyo
alikamatwa juzi akiwa katika harakati za kurejea Tanzania
wakati akitoka mapumziko nchini Brazil
ambapo mumewe alimpa nafasi ya kwenda likizo ya miezi mitatu ili
akapumzike."Wa k a t i n i k iwa k a t i k a mapumziko nchini Brazil, rafiki wa mumewe alinipa haya mabegi
niweze kurejea nayo Tanzania,"
alidai mwanamke huyo wakati akihojiwa na kuongeza kuwa;
"Mume wangu amenisababishia matatizo
kwa kunipa nafasi ya kupumzika miezi mitatu nchini Brazil," aliongeza.Hata hivyo,
mtandao huo ulidai mtuhumiwa huyo amepelekwa katika Mahakama ya Umma ili
taratibu za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake.