Aug 4, 2013

TUSIWARUHUSU WAVUNJE UMOJA WETU.MAALIM SEIF.


  • SILAHA YETU NI UMOJA.
Na mwandishi wetu wa munira.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,kwa mara nyengine amewaasa waislamu kuwa wamoja na katu wasiruhusu au kukubali kutenganishwa.

Amaeyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa anawasilimia Waumini walisowali Swala ya Ishaa katika Msikiti wa Qiblataini uliopo Kariakoo Jijini Dar es salaam.

Amesema “sisi waislamu silaha yetu ni umoja wa kweli,sasa tusikubali wala kuruhusu watugawe kwa lengo la kuuvunja umoja wetu”,mwisho wa kunukuu.

Awali katika salamu zake aliwaomba waislamu wauthamini Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao kwa mwaka unakuja mara moja.

“Kwa kufahamu umuhimu na thamani ya mwezi huu,mtume s.a.w.amesema lau umma wangu wangefahamu ubora unapoatikana ndani ya mwezi huu,basi wangetamani uwe mwaka mzima”.alisema.

Aidha Maalim Seif alijumuika na Waislamu hao katika swala ya Taraw