Aug 4, 2013

TAASISI YA MUNIIRA MADRASA YAANDAA “MUNIRA FAMILY DAY”.



  • NI FUTARI YA PAMOJA,
  • LENGO NI KUWAFARIJI WAJANE,YATIMA NA WAZEE.
  • BANK YA AMANA YAIPIGA JEKI

Na mwandishi wetu wa munirablog.
Taasisi ya Muniira Madrasa And Islamic Propagation Association yenye makazi yake Magomeni Makuti jijini Dar es salaam,imeandaa Futari ya pamoja waliyoipa  jina la siku ya wanafamilia wa munira (Munira Family Day).

Akiongea na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake leo hii,Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ustaadh Ally Salum Jongo amesema Futari hiyo itahusisha wajane,yatima,wazee,wazazi,wanafunzi na waalimu,aidha masheikh na watu mbalimbli watakuwepo Inshaa Allah.

“Sisi kila mwaka inapofika siku kama hii (yaani Jumamosi ya kwanza la kumi la tatu) huwa tunaandaa futari ya pamoja tuliyoipa jina la Munira Family Day kwa lengo la kuwafariji walengwa hawa (akimaanisha wajane,yatima,wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu)” .mwisho wa kumnukuu.

Tunawaomba waumini wa kiislamu tushrikianae pamoja kwa hali na mali ili wmisho wa siku walengwa wasijine kwamba wametengwa.

Akijibu swali la mwandishi wa munirablog aliyetaka kujuwa nguvu ya kufanya hivyo wameipata wapi.Ustaadh Ally alisema,unajuwa Taasisi yetu ni changa sana na haina vyanzo madhubuti vya mapato,mafanikio haya yanatokana na kujitolea kwa waalimu wenyewe,wazazi na wapenda kheri ambapo aliishukuru Bank ya AMANA kwa kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha hilo.

Futari hiyo ya pamoja itafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 3/08/2013 katika viwanja vya munira ambapo itatanguliwa na mawaidha yatakayo tolewa na Sheikh Walid Al had,huku Swala ya Maghrib itaongozwa na Sheikh Abdallah Haroun Nyumba.


USTAADH ALLY SALUM JONGO AKIWA OFISINI KWA MAZUNGUMZO NA MWANDISHI WA MUNIRABLOG.