Aug 25, 2013

KATIKA KUTOA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA KATIBA; MUSIWAAPISHE VIONGOZI KWA KUSHIKA MAS HAFU;



 SHEIKH MUHAMMAD ISSA.

Na mwandishi wetu;
Serikali imeshauriwa kutotumia Qur aan (Mas haf) katika kuwaapisha viongozi mbalimbali ili kulinda heshima ya kitabu hicho kitukufu na muongozo sahihi kwa waislamu.

Hayo yapo katika mapendekezo ya Rasimu ya Katiba ya Baraza la Katiba la Waislamu lililoandaliwa na Baraza Kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislam.


Akiwasilisha mapendekezo kutoka katika kundi la Masheikh ikiwa ni sehemu ya makundi maalumu yaliyogawanywa katika kuichambua Rasimu ya katiba,Sheikh Muhammad Issa alisema moja katika mapendekezo muhimu ya Baraza la Katiba la Waislamu kwa Tume ya katiba ni kuwa,iwepo katika katiba kipengele kisemacho “Waislamu wasilazimshwe kuapa kwa kushika Mas hafu (QUR AAN)”

“Tumelazimika kuyaweka mapendekezo haya kutokana na ukweli kwamba  inawezekana muapaji akawa hana Twahara,sasa kuishika au kukichukuwa kitabu hiki wakati hauna Twahara haya ni makosa makubwa sana kwa mujibu wa Uislamu”mwisho wa kumnukuu.

Zaidi ya maoni mia moja yamekusanywa leo hii katika kikao cha Baraza la Katiba la Waislamu lililofsnyika leo hii katika Viwanja vya Sabasaba ndani ya ukumbi wa ALLY HASSAN MWINYI,mbapo mbali ya mambo mengine  Waislamu kupitia Baraza hilo maoni yao yamesisitiza zaidi juu ya uhuru wa imani ya dini na udhibiti wa Tume ya majeshi.
 
VIONGOZI WA BARAZA LA KATIBA LA KIISLAM ;

 
 ENGENEER MCHOROPA AKIWASILISHA MAONI YA KUNDI LA WALEMAVU.
 
 
 SEHEMU YA WAUMINI WA KIISLAMU WALIOSHIRIKI MCHAKATO WA MAPENDEKZO YA RASIMU YA KATIBA LEO HII.