HUSSEIN NDIYALI;MKURUGENZI WA ELIMU NA MAFUNZO TIPSO.
- ADAMSON AND EDUCATIONAL PUBLISHERS YAWAPIGA JEKI;
Na
mwandishi wetu;
Wakuu wa
Shule na Walimu nchini wametakiwa kuwa na uzalendo katika kazi yao ikiwa ni moja ya njia ya kufikia malengo
ya mpango mpya wa Serikali unao julikana kwa jina la BIG RESULT NOW (MATOKEO
MAKUBWA SASA ).
Hayo
yamesemwa Leo hii na Atukuzwe Sanga ambae ni Mshauri mkuu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali
inayojulikana kwa jina la AMS EDUCATIONAL & SOCIAL PROBLEMS CONSULTANCY ya
Jijini Dar es salaam.
Bwana Sanga
ambaye alikuwa ni muwezeshaji katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa DUCE Chang'ombe jijini Dar es salaam alisema “sisi tukiwa ni sehemu
ya wadau wa elimu hapa nchini hakuna sababu ya kuimba mwimbo tusioujuwa maana
yake,bali tuna kila sasbabu ya kujuwa kwa undani maana ya BIG RESULT NOW mbao
ni mpango uliozinduliwa na Serikali mwezi June mwaka huu na kuzihususha sekta
sita ikiwemo sekta ya elimu”.
Aliendelea
kuwafahamisha wanasemina ya kwamba “Kuna mambo mengi yanayoambatana na haya katika
kufikia kilele cha mafanikio ya mpango huu,lakini suala la uzalendo wa kweli
kwa walimu wakuu na wakuu wa Shule,hili ni suala muhimu sana na hii itakuwa ni
nyezo ya kufikia mafanikio hayo”.
“Ukiwa na
uzalendo wa kweli nafsi yako haitokubali wewe binafsi au mwanafunzi wako kuwa
sehemu ya kikwazo cha kufikia mafanikio muliyojiwekea kwa maslahi ya shule na
utakuwa mbele kwa kutoa msaada kwa wanafunzi wako,lakini pia niwaambie kitu kimoja ni muhimu kila mwalimu kwa maana kila shule ikaandaa Result yake yenye kukidhi mahitaji kwa mujibu wa mazingira yanayo wazunguka”alisema.
Kwa upande
mwengine Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo wa Tanzania Islamic Primary School
Organization (TIPSO) Ndugu Hussein Ndiyali alisema wamefikia maamuzi ya kuwafanyia Semina Wakuu na Wamiliki wa Shule ili kuangalia tunawezaje kuitekeleza dhana ya
BRN,majukumu na wajibu wa walimu katika kuitikia wito wa Serikali juu ya dhana
ya BIG RESULT NOW na Changamoto zilizopo katika Shule za Kiislamu ambazo
zinaanza vizuri lakini hazisimami kileleni katika kuongoza.
Katika semina hiyo,jumla ya wamiliki na walimu wakuu wa shule wa mikoa mitatu waishiriki,mikoa hiyo ni Dar es salaam,pwani na morogoro.
Wakati huo
huo Mkurugenzi wa kampuni ya Adamson Educational Publishers ndugu Celestine
Adiema aliwaambia washiriki wa semina hiyo kwamba kampuni yake imeboresha vitabu
vyake na kuwataka wanachama wa TIPSO waendelee kutumia vitabu hivyo vyenye
ubora katika mashule yao.
Kampuni Adamson
Educational Publishers ndiyo iliyofanikisha kwa sehemu kubwa kufanyika semina hiyo.
ATUKUZWE SANGA,AKITOA MADA KATIKA SEMINA HIYO.
CELESTINE ADIEMA ,MKURUGENZI WA ADAMSON EDUCATIONAL PUBLISHERS,
NA HAPA CHINI NI SEHEMU YA VITABU VINAVYOTUNGWA NA KAMPUNI HIYO.