KUTOKA KUSHOTO NI,MHE SADIK MBWANA KADULO (MWENYEKITI JUMIYA YA WAZAZI KATA YA MAGOMENI),MHE SALUM KONDO MADENGE (MGENI RASMI),MHE SHWAJI ABDALLAH MKUMBULA,MWENYEKITI KATA YA MAGOMENI,MERINA VICTOR (KATIBU WA WAZAZI KINONDONI NA MARIAMU MUSSA (KATIBU WA WAZAZI KATA YA MAGOMENI)
- MAADILI MEMA YANAPOTOWEKA TAIFA HUWA HATARINI.
Na mwandishi wetu;
"Ndugu wajumbe,suala la maadili mema kwa vijana wetu tulipe
kipaumbele,kwani vijana wetu wakiwa na maadili mema ni wazi tutakuwa na taifa
lenye amani,taifa lenye vijana wenye afya bora na taifa lenye maendeleo taifa
ambalo litaheshimika mbele ya mataifa mengine"mwisho wa kumnukuu.
HABARI KAMAILI;
Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Magomeni,jana ilifanya mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Tawi la Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam.
Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Magomeni,jana ilifanya mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Tawi la Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mahojiano yaliyofanyika jioni hii kwa njia ya
simu,mjumbe wa elimu, uchumi,malezi na mazingira kata ya magomeni Ndugu Tewa
Ibrahim ameipasha munirablog ya kwamba,huo ulikuwa ni Mkutano Mkuu uliokuwa na Agenda za Uhai wa Jumuiya,taarifa ya kazi kwa mwaka 2012/2013 sambamba na mada
mbalimbali zilitolewa.
Akiongea katika mkutano huo,Mjumbe wa kamati ya utendaji wilaya
ya kinondoni ndugu Busolwa Pazi aliitaka jamii isimamie vilivyo maadili mema ya watoto ili
kuwa na Taifa lenye maendeleo.
"Ndugu wajumbe,suala la maadili mema kwa vijana wetu tulipe
kipaumbele,kwani vijana wetu wakiwa na maadili mema ni wazi tutakuwa na taifa
lenye amani,taifa lenye vijana wenye afya bora na taifa lenye maendeleo taifa
ambalo litaheshimika mbele ya mataifa mengine"mwisho wa kumnukuu.
Aliendelea kwa kusema "ndugu zangu,unapoona kuna taifa lenye mapigano,taifa lenye
maradhi au taifa lisilo na maendeleo,fahamu ya kwamba mbali ya mambo mengine
lakini watu wa taifa hilo
hawakuwa na maadili mema".
Kumekuwa na wimbi la matukio ya uhalifu yanayofanywa kwa asilimia kubwa na vijana ambapo inaaminika kwamba inasababishwa na ukosefu au upungufu wa maadili mema.
Wakati huo huo habari zilizotufikia hivi punde zinasema Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi imemvua Uanachama Mhe Mansuor Yusuf Himid kwa tuhuma za kukihujumu Chama hicho.
Kutokana na maamuzi hayo.Mhe Mansuor atakuwa amepoteza nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Kiembe Samaki Unguja Zanzibar.
WAZIRI WA NCHI,MAJI,NISHATI,ARDHI NA MAZINGIRA AMBAYE PIA NI MWAKILISHI WA KIEMBE SAMAKI MHE MANSOUR YUSUF HIMID,AMBAYE HIVI PUNDE KAVULIWA UANACHAMA WA CCM.