Aug 26, 2013

Hatimaye Mansour Yussuf Himid afukuzwa rasmi CCM.


  • Msimamo wake juu ya muungano wa mkataba wamponza.

  • Atafsriwa kua ni muhujumu wa chama.

Mwakilishi wa jimbo la kiembesamaki kupitia chama cha mapinduzi ndugu Mansour Yussuf Himid hatimaye amefukuzwa uanachama wa chama hicho akidaiwa kukisaliti kwa kuunga mkono muungano wa mkataba.Taarifa rasmi kutoka mjini Dodoma zinasema kuwa kikao cha halmashauri kuu ccm taifa kilichokutana kwa siku ya tatu chini ya mwenyekiti wake rais jakaya kikwete kimetoa uamuzi wa kufukuzwa kwa mwanachama huyo. Kufuatia hatua hiyo chama cha mapinduzi kitatoa taarifa kwa spika wa baraza la wawakilishi kuondoa udhamini wake kwa mwanachama huyo kama mjumbe wa baraza la wawakilishi wa jimbo kiembesamaki.
Hatua hiyo itamfanya spika wa baraza hilo kutangaza kiti cha jimbo hilo kuwa wazi na kuitishwa uchaguzi mdogo wa kugombea nafasi hiyo.

mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya ccm taifa daud ismail amesema kuwa Kikao hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kupokea madai ya mkoa wa magharibi kichama kutaka mwanachama huyo afukuzwe kwa madai ya kupinga sera ya serikali mbili za muungano inayoungwa mkono na chama hicho.
Kwa mujibu wa taratibu za ccm iwapo mansour hakuridhishwa na uamuzi wa kufukuzwa kwake anaweza kukata rufaa mahakama kuu kupinga uamuzi huo.