Sheikh.Ally Bassaleh akiwahutubia waislamu katika mashindano hayo. |
- TUWANYENYEKEENI NA TUWAUNGE MKONO.
- MASHINDANO YA QUR AAN YAFANA.
- ZAWADI ZA MAMILIONI YA PESA ZATOLEWA.
Na mwandishi wetu wa
munira.
Waislamu
wanetakiwa kuwa na silka ya kuwaheshimu,kuwapenda na kuwaunga mkono watoto
waliohifadhi Qur aan na kuacha tabia ya baadhi ya waislamu kuwahusudu watoto
hao kwa kuwaonea wivu.
Hayo yamesemwa
na Dokta Suleyman Ally Yusuph ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano ya
kuhifadhi qur aan yaliyomalizika hivi punde katika ukumbi wa diamond jubilee
uliopo upanga jijini dare s salaam.
Akiongea katika
hafla hiyo Dokta Suleyman ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kuhifadhi Qur
aan Tnzania amesema,Mtume S.A.W amekataza tabia ya kuwasimamia watu,lakini kwa
kuwa hawa watoto wamehifadhi Qur an yote tena miongoni mwao ni walemavu wa
macho,hawa inafaa kuwanyenyekea,naomba nieleweke,sipingani na maneno ya Mtume S.A.W
laa hashaa ,alisema.
“Leo badala ya
kuwapenda watoto kama hawa,au kufanya jitihada ili mtoto wako awe kama watoto hawa badala yake miongoni mwetu tunawahusudu
kwa njia mbalimbali”mwisho
wa kumnukuu.
Akiongea katika
hafla hiyo,Sheikh Ally Bassaleh alisema,”katika ulimwengu huu,Qur aan ndiyo kitabu
pekee chenye miujiza na hakuna kitabu chochote kinachoweza kuhifadhiwa chote
hata na watu wenye macho yao
sembuse walemavu wa macho,tumeshuhudia hivi punde watoto walemavu wa macho
wakiwa wamehifadhi qur aan kwa njia tofauti”.
Aliwanasihi
Waislamu wasiishie katika kuhifadhi pekee bali pia wazingatie yaliyomo katika
qur aan.
Katika mashindano
hayo zawadi za pesa na vitu mbalimbali ikiwemo Vyarahani,Pikipiki,Bajaji,Baiskeli
zilitolewa kwa washindi,ambapo Abdul hamiid Masuod alifanikiwa kuwa mshindi wa
kwanza kwa wanaume waliohifadhi Juzuu 30
ambapo alipata pesa taslimu Shilingi Laki tatu na Bajaji,sambamba na suraiyyah
ally baker mshindi wa kwanza kwa wanawake ambaye pia alipata bajaji na pesa
taslimu shilingi laki tatu.
”Namshukuru
mungu ameniwezesha kufikia malengo yangu,hii pesa nitaitumia katika
kujiendeleza na elimu ya kimazingira (shule) na hii Bajaji nitaifanya kuwa ni
kitega uchumi”,aliongea Abdul hamiid Masuod mbaye ni Mwanafunzi katika
Madrasat Baytul Maqdis ya Ubungo
Taasisi ya
Aisha Sururu Foundation chini ya Mkurugenzi Mtendaji Bi Aisha Sururu ndiyo Taasisi
iliyoandaa mashindano hayo,na huu ni mwaka wa saba mfululizo toka waanzishe
mashindano hayo.
MABRUOK A'LAYK"NDIVYO ANAVYONEKANA KUSEMA MGENI RASMI WAKATI AKIMKUMBATIA MSHINDI WA KWANZA WA JUZUU 30 KWA UPANDE WA WANAUME KIJANA ABDUL HAMIID MASOUD KUTOKA UBUNGO JIJIN DAR ES SALAAM.
MHE MGENI RASMI AKIMKABIDHI ABDUL HAMIID MASUOD (MSHINDI WA KWANZA WA JUZUU 30) KITITA CHA PESA NA BAJAJI.
"KWA KWELI SIWEZI KUZUNGUMZA,KWANI NIMECHOKA SANA NA NINA FURAHA KUPITA KIASI,ILA NAMSHUKURU MUNGU MAMBO YAMEENDA VIZURI,NDIVYO ALIVYOSEMA BI AISHA SURURU ALIPOTAKIWA KUFANYA MAHOJIANO NA MWANDISHI WA MUNIRABLOG LEO HII.
MHE MGENI RASMI AKIMKABIDHI ABDUL HAMIID MASUOD (MSHINDI WA KWANZA WA JUZUU 30) KITITA CHA PESA NA BAJAJI.
"KWA KWELI SIWEZI KUZUNGUMZA,KWANI NIMECHOKA SANA NA NINA FURAHA KUPITA KIASI,ILA NAMSHUKURU MUNGU MAMBO YAMEENDA VIZURI,NDIVYO ALIVYOSEMA BI AISHA SURURU ALIPOTAKIWA KUFANYA MAHOJIANO NA MWANDISHI WA MUNIRABLOG LEO HII.
PICHA JUU NI BINTI ALIYEHIFADHI JUZUU KUMI KATIKA MTINDO WA TAHQIIQ HALI YA KUWA NI MLEMAVU WA MACHO NA MIGUU NA MIKONO,ALLAHU AKBAR
PICHA CHINI NI MSHINDI WA TATU WA JUZUU KUMI BI ASIA MUHUNZI FAQIH (UMRI MIAKA 8) AKIWA AMESHIKILIA KITITA CHA SHILINGI LAKI SITA ZIKIWA NI ZAWADI ZA USHINDI WAKE,AMEMUELEZA MWANDISHI WA MUNIRABLOG KWAMBA HAJUWI ATAZIFANYIA NINI PESA HIZO ILA HATOMPA BABA WALA MAMA BALI ATAMPA USTAADH WAKE WA MADRSAT JAWHARIYYAH YA VINGUNGUTI,DAR ES SALAAM